131. Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi Yake

25 – Bukayr bin Ja´far as-Sulamiy, mmoja katika wanazuoni wa Jurjaan.

166 – Abu Ahmad bin ´Adiy, nataraji kuwa hana neno, ameeleza kutoka kwa Ibrahiym bin Muusa, ambaye amesema:

”Wakati nilipokuwa kwa Bukayr bin Ja´far alikuja bwana mmoja na kusema: ”Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake; vipi?” Bukayr akasema: ”Mshikeni mguu wake na mumvute.” Wakamvuta.”[1]

28 – Haafidhw Bishr bin ´Umar az-Zahraaniy (d. 207).

167 – ´Umar bin Shayruuyah amesema: Nimemsikia Ishaaq bin Raahuuyah: Bishr bin ´Umar ametueleza:

”Nimewasikia wafasiri wengi wa Qur-aan wakisema kuhusu:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[2]

”Bi maana Yuko juu ya ´Arshi.”[3]

29 – Yahyaa al-Qattwaan (120-198), bingwa wa wenye kuhifadhi.

168 – Abu Haatim ar-Raaziy amesema: ´Abbaas al-´Anbariy amenihadithia: Nimemsikia Abul-Waliyd at-Twayaalisiy: Yahyaa bin Sa´iyd amesema:

”Itakuweje:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.”[4]

Wanasema kuwa imeumbwa?”[5]

[1] Ibn ´Adiy ameitaja katika wasifu wake katika ”al-Kaamil” na akasema:

”Nataraji kuwa hana neno.”

Kupitia kwake mtunzi (Rahimahu Allaah) ameisimulia. Ibn ´Adiy amesema: Muhammad bin ´Umar ametukhabarisha: Nimemsikia Muhammad bin Yuusuf al-Istirbaadhiy: Nimemsikia Ibraahiym bin Muusa.

Simjui ni nani huyu Muhammad bin ´Umar.

[2] 20:05

[3] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh na iko na wasimulizi madhubuti na wenye kuhifadhi. Ishaaq bin Raahuuyah alikuwa ni imamu mwenye kutambulika na madhubuti ambaye alikuwa katika rika la Imaam Ahmad. ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan bin Shayruurah bin Asad al-Qurashiy al-Matwlabiy an-Naysaabuuriy pia alikuwa madhubuti na mwenye kuhifadhi. Imekuja katika “Shadharaat-udh-Dhahab” (2/246):

”Ni mmoja katika wale wenye kuhifadhi. Alikuwa ni katika rika la Ishaaq bin Raahuuyah, Ahmad bin Maniy´ na rika lao. Aliandika vitabu na alikuwa madhubuti.”

[4] 112:1

[5] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. ´Abdullaah bin Ahmad ameipokea katika ”as-Sunnah”, uk. 26, kwa tamko lisemalo:

”Yahyaa bin Sa´iyd amenambia: ”Wanachukua msimamo gani kwa:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.” (112:1)?

Wanachukua msimamo gani kwa Aayah hii:

إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ

”Hakika mimi ni Allaah.” (20:14)?

Imeumbwa?”

al-Bukhaariy ameitaja katika “Khalqu Af´aal-il-´Ibaad”, uk. 69-70, kwa cheni ya wapokezi pungufu kutoka kwa Abul-Waliyd.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 153-154
  • Imechapishwa: 22/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy