Kwa hivyo kutokana na yaliyotangulia inapata kufahamika kwamba haifai kusema kuhusu Uislamu na unaswara yale yaliyosemwa na mwandishi kwa njia ya kuachia pale aliposema:

“Kwa ajili hiyo ni lazima kwetu tuepuke mizozo aina yote kati ya dini hizo mbili na tufanye kuwe na mapatano kati ya waislamu na manaswara katika kumtumikia mwanadamu.”

Unaswara sio dini yetu. Dini yetu ni Uislamu peke yake. Kuhusu unaswara tayari imekwishatangulia kwamba ni dini batili na ile haki iliyomo ndani amekuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kwa yale ambayo ni timilifu zaidi kuliko hayo. Hivyo waislamu watayatendea kazi kwa sababu ni miongoni mwa Uislamu ambao Allaah amemtumiliza kwao Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawayatendei kazi kwa sababu yamekuja ndani ya Tawraat na Injiyl. Bali ni kwa sababu Shari´ah yetu ya Uislamu imekuja nayo na kulingania kwayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 07/10/2021