13. Njia ya sita: kutilia bidii na kujishughulisha na vitabu vya Salaf

Miongoni mwa njia za kuifikia elimu ni kujishughulisha na vitabu vya Salaf na kupuuza vitabu vingine ambavyo vinashughulisha na havifidishi. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba vitabu vya Salaf vimejaa kheri zote na hautofaulu mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa yale waliyofaulu kwayo wa mwanzo wao. Yaliyowafanya wafaulu wa mwanzo wa Ummah huu ni yale waliyoandika Salaf katika vitabu vyao.

Hivyo inatakikana kwa mwanafunzi ajishughulishe na vitabu vya Salaf na asijali vitabu vya sasa ambavyo vinamshughulisha mwanafunzi kutokana na wakati wake na vinampotezea wakati wake mwingi.

Baadhi ya wanafunzi wanawapenda waandishi waliokuja nyuma na wanawaacha waandishi wa kale. Kadhalika wanapupia vitabu vya waliokuja nyuma. Hakika kwa kufanya hivo wanaweza kupitwa na kheri nyingi. Simaanishi kuwa mwanafunzi asisomi vitabu vya waliokuja nyuma. Ninachomaanisha ni kwamba asijishughulishe sana nafsi yake na vitabu vya waliokuja nyuma. Anatakiwa kujishughulisha na kutilia bidii kubwa vitabu vya Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Kuhusu vitabu vya waliokuja nyuma achague vile ambavyo ni vizuri ijapokuwa ni vichache. Pamoja na hivyo asijishughulishe navyo sana. Atosheke na kusoma yale yenye kumnufaisha, kumpa faida na kumtengeneza katika dini yake. Ama kinachomfikisha mtu katika elimu ya sawasawa ni yeye kujishughulisha na vitabu vya as-Salaf as-Swaalih.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016