Amesema (Ra´aahu Allaah) katika kusifu kwake kitabu “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat”:
“Muheshimiwa Shaykh, ´Allaamah, Ustadhw na Dr. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy amemraddi ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq baada ya kutumia muda na juhudi kubwa kumnasihi kwa siri na kwa dhahiri. Amefanya hivo kwenye kitabu kwa anwani “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat wa Swiraatw Waahidah laa ´Aisharaat”. Nimesoma kitabu chote na nimeona kuwa ni chenye manufaa, thamani na chenye kutimiza malengo ya ni kwa nini kimeandikwa. Humo kuna uwakilisho na uchambuzi makini juu ya maneno ya ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq ambayo yanapatikana katika kanda na vitabu vyake. Amebainisha uongo wa maneno hayo kwa hoja na dalili za wazi kabisa. Amefanya hili kwa amana ya kielimu na uthibitishaji katika vitabu vyake na vyanzo. Amenasihi Ummah mzima kwa jumla na khaswa Shaykh ´Abdur-Rahmaan kushikamana barabara na mfumo wa wema waliotangulia pamoja kuraddi mifumo yote inayoenda kinyume na Kitabu na Sunnah. Kwani Uislamu ni njia moja na ni mfumo mmoja. Amesema (Ta´ala):
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ
“Kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni – na wala msifuate njia za vichochoro nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo alivyokuusieni kwayo mpate kumcha.” (06:153)
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ
“Tuongoze njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.” (01:06-07)
وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا
”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!” (04:115)
Kitabu hichi kikubwa ambacho ndani yake Shaykh Rabiy´ amebainisha kwa ufafanuzi ni kitabu ambacho mwanafunzi hatakiwi kukikosa. Hili kwa sababu awe ni mwenye bayana na ili utata uliokakamana kwenye kucha za watu wengi uweze kutoweka. Utata huu unatokamana na mifumo hii ya makosa, ni yenye kung´aa, lakini ni mitupu, ina kauli mbiu pamoja na hila katika usulubu.
Hii kazi kubwa ambayo muheshimiwa Shaykh Rabiy´ (Hafidhwahu Allaah) amesimama nayo ni moja katika michango mingi aliyotoa ili kuinusuru Dini, kutetea Sunnah, kuilinda ´Aqiydah na kufichukua upotevu wa Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´. Amefanya hilo kwa njia ya kielimu na imara na mfumo wa usawa. Amebainisha hilo kupitia njia ya vitabu vyake vyenye thamani, mihadhara yake yenye faida na kuwatilia umuhimu vijana na kuwaelekeza katika mfumo wa haki. Anatumia wakati wake wote kuitumikia elimu na kutangamana na wanafunzi zake pamoja na matatizo yote yanayomkabili na khaswa kutoka kwenye makundi hayo ya vyama yaliyopetuka mipaka ambao wao walengwa wao ni wanachuoni, wanafunzi na Salafiyyuun. Wanawachafua kwa uvumi wa batili, uongo, udanganyifu, utatizi na kuyapotosha maneno kuyatoa mahala pake stahiki. Kwa watu kama hawa na mfano wao nawaambia yafuatayo:
Bahari iliyojaa haidhuriki kwa
Kijana mdogo anayejitupa ndani yake
فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً ۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ
“Basi povu la takataka linapita bure bila ya kufaa. Lakini vile vinavyowafaa watu hubakia ardhini.” (13:17)
Allaah Amjaze Shaykh Rabiy´ kwa juhudi hii kubwa kheri kwa njia Aliyowapa waja Wake wema na Afanye juhudi hizi ziwe ni zenye uzito mkubwa katika mizani yake – hakika Yeye yukaribu na ni Mwenye kujibu.”[1]
[1] Tazama dibaji ya kitabu cha Shaykh Rabiy´ ”an-Naswr al-´Aziyz”.
- Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
- Imechapishwa: 05/12/2019

Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
Imechapishwa: 05/12/2019
https://firqatunnajia.com/13-muheshimiwa-shaykh-swaalih-bin-sad-as-suhaymiy-hafidhwahu-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)