13. Msingi wa nne: ulazima wa kuwatii watawala wa kiislamu katika mema

Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba ni wajibu kuwatii watawala wa waislamu midhali hawajaamrisha maasi. Wakiamrisha maasi itakuwa haijuzu kuwatii. Lakini hata hivyo mtu atabaki kuendelea kuwatii katika mema mengine. Hilo ni kwa sababu ya kutendea kazi maneno Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nakuusieni kumcha Allaah na kusikia na kutii hata kama mtatawaliwa na mja.”[2]

Wanaona kuwa kumuasi mtawala wa kiislamu ni kumuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanafanya hivo kwa kutendea kazi maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kumtii kiongozi amenitii mimi na yule mwenye kumuasi kiongozi ameniasi mimi.”[3]

Wanaonelea kuswali nyuma yao, kupigana Jihaad bega kwa bega pamoja na wao, kuwaombea du´aa ya kutengemaa, kunyooka na kuwanasihi.

[1] 04:59

[2] Abu Daawuud (4609), at-Tirmidhiy (2676), Ibn Maajah (46) na Ahmad (17184)

[3] al-Bukhaariy (2797), Muslim (1835), an-Nasaa´iy (4193), Ibn Maajah (3859) na Ahmad (03/387)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Usuwl ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 12/05/2022