12. Mitume ni wakweli katika yale waliyoeleza juu ya Allaah

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Halafu Mitume Wake ni wakweli na ni wenye kusadikishwa, tofauti na wale wanaosema juu Yake yale wasioyajua. Na kwa ajili ya hii ndio maana amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Ametakasika Mola wako, Mola Mtukufu kutokana na yote wanayoelezea na amani iwe juu ya Mitume na himidi zote ni za Mola wa walimwengu.” (37:181-182)

Hiivyo amejitakasa nafsi Yake kutokana na yale waliyomuelezea kwayo wale waendao kinyume na Mitume na akawatakia amani Mitume Yake kuthibitisha kusalimika yale waliyoyasema kutokamana na mapungufu na kasoro.

MAELEZO

Amesema (Rahimahu Allaah):

“Halafu Mitume Wake ni wakweli na ni wenye kusadikishwa, tofauti na wale wanaosema juu Yake yale wasioyajua.”

Kisha Mitume Yake pia ni wakweli na ni wenye kusadikishwa katika yale waliyoelezea. Yale ambayo Qur-aan inaelezea Mitume pia (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) wameyaelezea. Mbora wao, kiongozi wao na wa mwisho wao ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ameeleza kuwa Yeye (Subhaanah) ndiye Yuko juu kabisa, amelingana juu ya ´Arshi, Yeye ndiye mwenye kutoa na kuzuia, Yeye ndiye ambaye juu ya kila kitu ni Muweza na kwamba Yeye ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa. Sunnah imetaja sifa Zake kuu (Subhaanah) na kwamba Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Mungu anayestahiki kuabudiwa. Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) ni wakweli katika yale waliyoelezea juu ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 17/10/2024