Baadhi ya watu wanakwenda kinyume na mwenendo wa Shari´ah katika daku na futari. Kuna kundi la watu, au wengi wao, wanakesha usiku na ikifika mwisho wa usiku wanapotaka kulala hula daku kabla ya alfajiri, kisha wanalala na wanaacha swalah ya Fajr kwa wakati wake pamoja na mkusanyiko. Hivyo wanakuwa wametenda makosa kadhaa:

1 – Wameanza kufunga kabla ya wakati wa kufunga.

2 – Wanaacha Fajr pamoja na mkusanyiko.

3 – Wanachelewesha swalah kutoka wakati wake na hivyo hawaiswali mpaka waamke, hata kama ni wakati wa Dhuhr.

Wazushi huchelewesha kufugnua swawm baada ya kuzama kwa jua na hawali isipokuwa baada ya nyota kuchomoza. Mwongozo bora ni mwongozo wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uou wa mambo ni yale yaliyozuliwa na kila Bi´ah ni upotofu.

Tunamuomba Allaah aturuzuku kushikamana na Sunnah na kujiepusha na Bid´ah na Ahl-ul-Bid´ah.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 21
  • Imechapishwa: 02/02/2026