69 – Tambua ya kwamba hakuna yeyote atayeingia Peponi isipokuwa kwa huruma ya Allaah, na kwamba Allaah hatomuadhibu yeyote isipokuwa kwa kiwango cha madhambi yake. Lau Allaah angeliwaadhibu walioko mbinguni, walioko ardhini, wema na waovu wao, basi angelikuwa ni mwenye kuwaadhibu pasi na kuwadhulumu. Haijuzu kumwambia Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) kwamba ni mwenye kudhulumu. Mwenye kudhulumu ni yule anayechukua kisichokuwa chake, ilihali Allaah (Jalla Thanaa´uh) viumbe na amri vyote viwili ni Vyake. Viumbe ni Wake na ulimwengu pia ni Wake. Haulizwi kwa kile anachokifanya na wao viumbe wataulizwa. Hakusemwi “Kwa nini?” wala “Vipi?”. Asiwepo yeyote atayeingia kati ya Allaah na viumbe Wake.
70 – Ukimsikia yeyote anayasema vibaya masimulizi na wala hayakubali au anapinga kitu chochote katika maelezo yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi utuhumu Uislamu wake. Huyo ni mtu aliye na maoni na ´Aqiydah mbovu. Hakufanya jengine zaidi ya kumtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, kwa sababu tumemjua Allaah, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Qur-aan, mambo ya kheri na mambo ya shari pamoja na ulimwengu na Aakhirah kupitia masimulizi.
71 – Qur-aan ni yenye kuihitajia zaidi Sunnah kuliko Sunnah inavyoihitajia Qur-aan.
72 – Maneno, mabishano na magomvi, na khaswa inapokuja katika makadirio, ni jambo limekatazwa kwa mujibu wa mapote yote, kwa sababu makadirio ni siri ya Allaah. Isitoshe Mola (Tabaarak wa Ta´ala) amewakataza Mitume kuzungumza juu ya makadirio. Vilevile Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuzozana juu ya makadirio. Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walichukizwa na jambo hilo na kadhalika wanafunzi wao. Vivyo hivyo ndivyo walivyofanya wanazuoni na wenye kumcha Allaah. Wao pia walikataza kubishana juu ya makadirio. Kwa hivyo ni juu yako kujisalimisha, kuthibitisha na kuamini yale aliyosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yanyamazie yasiyokuwa hayo.
73 – Inatakiwa kuamini ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisafirishwa usiku kuelekea mbinguni na akafika katika ´Arshi. Akazungumza na Allaah (Tabaarak wa Ta´ala), akaingia Peponi na akauona Moto. Akawaona Malaika na akayasikia maneno ya Allaah (´Azza wa Jall). Mitume walihuishwa kwa ajili yake. Aliona mabanda ya ´Arshi, Kursiy na vyote vilivyomo mbinguni na ardhini hali ya kuwa macho. Jibriyl ndiye alimbeba juu ya Buraaq mpaka akafika mbinguni. Katika usiku huo ndio alifaradhishiwa swalah na akarudi Makkah katika usiku huohuo. Hayo yalifanyika kabla ya Kuhajiri.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 88-90
- Imechapishwa: 18/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 88-90
Imechapishwa: 18/12/2024
https://firqatunnajia.com/13-makatazo-ya-mabishano-ya-kidini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)