13 – Kulingania kwa Allaah
Dada wa dini na imani, kuwa ni mlinganiaji kwa Allaah kwa utambuzi. Hiyo ndio njia ya mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ
“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata. Utakasifu ni wa Allaah na mimi si miongoni mwa washirikina.”[1]
Ambaye analingania kwa Allaah ana ujira mkubwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anayelingania kwenye uongofu basi anapata sawa na ujira wa yule atakayemfuata pasi na kupungua chochote katika ujira wao.”[2]
”Endapo Allaah atakuongozea mtu mmoja tu ni kheri kwako kuliko kupata ngamia wekundu.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Ukimlingania mwanamke mwenzako unapata ujira. Akiyafanyia kazi uliyomwambia basi unapata ujira sawasawa na malipo yake pasi na kupungua chochote katika ujira wake. Pengine ukajiuliza mwenyewe: vipi utalingania kwa Allaah? Tunakuambia: Si lazima uwe fasaha na mwenye balagha katika mazungumzo, lakini kwa kadiri ya uwezo. Ulingano unakuwa kwa maneno mazuri, kupeana zawadi ya kaseti yenye manufaa, zawadi, kijitabu, makala na mfano wake. Ninaapa kwa Allaah jambo hili lina fadhilah kubwa. Kwa hivyo usilipuuze.
[1] 12:108
[2] Muslim.
- Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 18-19
- Imechapishwa: 11/02/2026
13 – Kulingania kwa Allaah
Dada wa dini na imani, kuwa ni mlinganiaji kwa Allaah kwa utambuzi. Hiyo ndio njia ya mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ
“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata. Utakasifu ni wa Allaah na mimi si miongoni mwa washirikina.”[1]
Ambaye analingania kwa Allaah ana ujira mkubwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anayelingania kwenye uongofu basi anapata sawa na ujira wa yule atakayemfuata pasi na kupungua chochote katika ujira wao.”[2]
”Endapo Allaah atakuongozea mtu mmoja tu ni kheri kwako kuliko kupata ngamia wekundu.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Ukimlingania mwanamke mwenzako unapata ujira. Akiyafanyia kazi uliyomwambia basi unapata ujira sawasawa na malipo yake pasi na kupungua chochote katika ujira wake. Pengine ukajiuliza mwenyewe: vipi utalingania kwa Allaah? Tunakuambia: Si lazima uwe fasaha na mwenye balagha katika mazungumzo, lakini kwa kadiri ya uwezo. Ulingano unakuwa kwa maneno mazuri, kupeana zawadi ya kaseti yenye manufaa, zawadi, kijitabu, makala na mfano wake. Ninaapa kwa Allaah jambo hili lina fadhilah kubwa. Kwa hivyo usilipuuze.
[1] 12:108
[2] Muslim.
Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 18-19
Imechapishwa: 11/02/2026
https://firqatunnajia.com/13-kuwa-ni-mlinganizi/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket