6 – Kusherehekea maulidi ni alama yenye kujulisha kumpenda na ni moja katika alama yake. Kitendo cha kudhihirisha mapenzi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Tunajibu hilo kwa kusema ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo la wajibu kwa kila muislamu. Ni wajibu kwa kila muislamu kumpenda zaidi ya anavyojipenda yeye mwenyewe, mtoto wake, baba yake na watu wote. Hata hivyo hilo halina maana ya sisi kuzua kitu ambacho hatukuwekewa katika Shari´ah. Kumpenda kunapelekea kumtii na kumfuata. Hiyo ni moja katika alama kubwa za kumpenda. Mshairi amesema:
Lau mapenzi yako yangelikuwa ya kweli ungelimtii
hakika ya mwenye kupenda juu ya anayempenda humtii
Kumpenda yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunapelekea mtu akazihuisha Sunnah zake, kuziuma kwa magego na kujiepusha na maneno na matendo yanayoenda kinyume nazo. Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote kila kinachoenda kinyume na Sunnah zake ni Bid´ah yenye kusimangwa na ni maasi ya wazi kabisa. Katika hayo kunaingia pia kusherehekea kuzaliwa kwake na Bid´ah nyinginezo. Mtu kuwa na nia nzuri hakuhalalishi kuzua ndani ya dini. Dini imejengwa juu misingi miwili:
1 – Kumtakasia nia Allaah.
2 – Kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Amesema (Ta´ala):
بَلَى مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ
“Sivyo hivyo! Yeyote anayeelekeza uso wake kwa Allaah naye ni mtenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola Wake, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.”[1]
Kuusalimisha uso ndio kumtakasia nia Allaah, na wema ni kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuafikiana na Sunnah.
[1] 02:112
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 155-156
- Imechapishwa: 06/09/2025
6 – Kusherehekea maulidi ni alama yenye kujulisha kumpenda na ni moja katika alama yake. Kitendo cha kudhihirisha mapenzi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Tunajibu hilo kwa kusema ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo la wajibu kwa kila muislamu. Ni wajibu kwa kila muislamu kumpenda zaidi ya anavyojipenda yeye mwenyewe, mtoto wake, baba yake na watu wote. Hata hivyo hilo halina maana ya sisi kuzua kitu ambacho hatukuwekewa katika Shari´ah. Kumpenda kunapelekea kumtii na kumfuata. Hiyo ni moja katika alama kubwa za kumpenda. Mshairi amesema:
Lau mapenzi yako yangelikuwa ya kweli ungelimtii
hakika ya mwenye kupenda juu ya anayempenda humtii
Kumpenda yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunapelekea mtu akazihuisha Sunnah zake, kuziuma kwa magego na kujiepusha na maneno na matendo yanayoenda kinyume nazo. Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote kila kinachoenda kinyume na Sunnah zake ni Bid´ah yenye kusimangwa na ni maasi ya wazi kabisa. Katika hayo kunaingia pia kusherehekea kuzaliwa kwake na Bid´ah nyinginezo. Mtu kuwa na nia nzuri hakuhalalishi kuzua ndani ya dini. Dini imejengwa juu misingi miwili:
1 – Kumtakasia nia Allaah.
2 – Kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Amesema (Ta´ala):
بَلَى مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ
“Sivyo hivyo! Yeyote anayeelekeza uso wake kwa Allaah naye ni mtenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola Wake, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.”[1]
Kuusalimisha uso ndio kumtakasia nia Allaah, na wema ni kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuafikiana na Sunnah.
[1] 02:112
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 155-156
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/13-kusherehekea-maulidi-ni-alama-ya-kumpenda/