Swali 13: Kuna baadhi ya Hadiyth ambazo baadhi ya watu wanazitumia kuthibitisha kwamba mwenye kuacha matendo yote kabisa bado ni muumini mwenye upungufu wa imani. Mfano wa Hadiyth ni zifuatazo:
”… ambaye hakuwahi kufanya wema wowote kabisa.”
na Hadiyth ya yule bwana wa kadi. Wanajibiwa vipi?
Jibu: Hakuna hoja yoyote katika Hadiyth hizi kwa yule anayedai hivyo. Mtu anayeacha matendo yote kabisa na kudai kuwa anatosheka tu na yakini ya moyo, basi imani yake haithibiti isipokuwa kwa matendo. Ama kuhusu Hadiyth za nyombezi na kwamba waumini waliokuwa wakimwabudu Allaah pekee watafanyiwa maombezi na Mitume, watoto waliokufa kabla ya kubaleghe, waliokuwa hali ya kuwa ni mashahidi, Malaika, waumini na bado watabakia wengine ambao hawatopata uombezi ambapo ndipo Allaah atawatoa kwa rehema Yake na kwamba atawatoa watu kutoka Motoni ambao hawajapatapo kufanya kheri yoyote, wanazuoni wamesema kuwa maana yake ”hawajapatapo kufanya kheri yoyote” inayozidi juu ya Tawhiyd na imani. Ni lazima iwe hivo, kwa sababu maandiko yanapaswa kuoanishwa. Dalili za Qur-aan na Sunnah zimefahamisha ya kwamba Pepo ni haramu kwa washirikina. Aidha katika Hadiyth sahihi imethibitika kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwabudu mtangazaji atangaze katika baadhi ya vita:
“Hakika hataingia Peponi isipokuwa nafsi yenye imani.”
Alipomfanya Abu Bakr kuwa kiongozi wa hijjah katika mwaka wa tisa baada ya kuhajiri, alimwagiza pamoja na watangazaji wengine akiwemo Abu Hurayrah, wawatangazie watu mambo manne ikiwa ni pamoja na:
“Hataingia Peponi isipokuwa nafsi yenye imani, baada ya mwaka huu asihiji mshirikina yeyote, asitufu yeyote kwenye Ka‘bah akiwa uchi, mwenye mkataba wa amani atabaki katika ahadi yake na asiye na mkataba ana muda wa miezi minne.”
Hili linathibitisha kuwa haiwezekani kwa kafiri yeyote kuingia Peponi. Amesema (Ta´ala):
إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ
“Hakika yule atakayemshirikisha Allaah, basi hakika Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni motoni – na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kuwanusuru.”[1]
Hivyo hizi ni dalili zilizo wazi. Hadiyth isiyo wazi inarudishwa katika maandiko yaliyo wazi. Kanuni kwa wanazuoni ni kwamba maandiko yasiyo wazi yanarudishwa katika maandiko yaliyo wazi. Hakuna anayeshikamana na dalili zenye utata na zisizo wazi isipokuwa tu wapotofu. Amesema (Ta´ala):
فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ
”Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotevu hufuata zile zisizokuwa wazi ili kutafuta fitina na kutafuta kuzipotosha.”[2]
Imethibiti katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba ‘Aaishah amesema:
“Mkiwaona wale wanaofuata yaliyo yenye kutatiza katika hiyo [Qur-aan], basi hao ndio wale ambao Allaah amewataja. Jihadharini nao.”
Watu wa haki wao wanarejesha dalili zenye kutatiza kwenda katika zile zilizo wazi na wanazifasiri kwa mujibu wake. Hadiyth hii ina tatiza na ndio maana inatakiwa kurejeshwa katika yale maandiko yaliyo wazi yanayosema kwamba mshirikina hatoingia Peponi na kwamba Pepo imeharamishwa kwake. Kwa hivyo maana ya Hadiyth:

haiwezekani kwamba ni washirikina wasiokuwa na Tawhiyd wala imani kisha Allaah awatoe Motoni na kuwaingiza Peponi. Bali maana yake ni kuwa hawakuwahi kufanya wema wowote zaidi ya Tawhiyd na imani. Vivyo hivyo Hadiyth ya kadi haijatajwa kuwa mtu huyu alikuwa mshirikina, bali alikuwa mwenye Tawhiyd. Hadiyth inasema:
“Mtu ataletewe daftari tisini na tisa yaliyojaa madhambi. Kisha ataletewe kadi yenye shahaadah mbili na kadi itawekwa upande mmoja wa mizani na daftari hizo upande mwingine na daftari zote zitakuwa nyepesi huku kadi ikawa nzito.”
Ni jambo linalojulikana ya kuwa kila muislamu ana kadi hii ya shahaadah na mengi zaidi, ingawa baadhi yao wataingia Motoni. Lakini bwana huyu alipotamka shahaadah hizi mbili alifanya hivo kwa kumtakasia nia Allaah, ukweli na kujutia na hivyo yakachoma madhambi hayo na hivyo kadi ikawa nzito na kufuta madhambi yote.
[1] 05:72
[2] 03:07 Ameipokea al-Khatwiyb katika wasifu wa Mansuur kwenye “Taariykh Baghdaad” (13/75-76) kupitia kwa Abu ´Aliy al-Husayn bin al-Qaasim al-Kawkabiy: Jariyr bin Ahmad bin Abiy Du-aad Abu Maalik ametuhadithia: Hakimu wa Hijr Sulmuuyah bin ´Aaswim, ambaye alifanya kazi katika bara arabu na Shaam, amenihadithia.
Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Haafidhw Ibn Hajar amesema kuhusu al-Kawkabiy:
”Msimulizi wa khabari zinazojulikana. Nimeona akisimulia masimulizi mengi dhaifu na yenye kugongana yakiwa na cheni za wapokezi nzuri.” (Lisaan-ul-Miyzaan)
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 32-35
- Imechapishwa: 06/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 32-35
Imechapishwa: 06/01/2026
https://firqatunnajia.com/13-je-kuna-hadiyth-zinazofahamisha-kwamba-anayeacha-matendo-kabisa-bado-ni-muuni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket