49 – Abul-Hasan Muhammad bin ´Abdillaah bin Muhammad al-Hinnaa-iy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ahmad bin as-Swiddiyq al-Marwaziy ametuzindua: Abu Lubaabah Muhammad bin al-Mahdiy ametukhabarisha: Ahmad bin ´Abdillaah bin Hakiym ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin Ahmad bin Ja´far al-Yazdiy amenikhabarisha huko Aswbahaan: Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Atwaa al-Qabbaab ametuhadithia: Abu Twaalib ´Abdullaah bin Ahmad bin Sawaadah al-Baghdaadiy ametuhadithia kwa njia ya kutusomea: al-Hasan bin Qaz´ah ametuhadithia: al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw ametuhadithia… (ح) al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Abu Muhammad Da´laj bin Ahmad bin Da´laj al-Mu-addil ametuzindua: Muhammad bin ´Aliy bin Zayd as-Swaa-igh ametuzindua: Sa´iyd bin Mansuur ametuhadithia: Fudhwayl bin ´Iyaadhw ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin ´Abdillaah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Enyi ummah! Mimi sichelei juu yenu kwa yale msiyoyajua, lakini tazameni ni vipi mnatendea kazi yale mliyojifunza.”[1]

50 – Abu ´Aliy al-Hasan bin al-Husayn bin al-´Abbaas an-Ni´aaliy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Ibraahiym al-Marwaziy ametuhadithia: Abu ´Abdir-Rahmaan ´Abdullaah bin Mahmuud ametuhadithia: Yahyaa bin Aktham ametuhadithia: ´Abdul-A´laa bin Mushir al-Ghassaaniy ametuhadithia: Nimemsikia Khaalid bin Yaziyd bin Swubayh akisema: Nimemsikia Yuunus bin Maysarah bin Halbas al-Jublaaniy akisema:

”Hekima inasema: ”Ee mwanadamu, unanitamani, lakini unaweza kunipa kwa njia fulani: ifanyia kazi ile kheri ya uliyojifunza na jiepushe na shari ya uliyojifunza.”

51 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Abu Sahl Ahmad bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Ziyaad al-Qattwaan ametuzindua: ´Abdul-Kariym bin al-Haytham ametuhadithia: Abul-Yamaan ametuhadithia: Hariyr ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Abiy ´Awf, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:

”Mja siku ya Qiyaamah ataulizwa: ”Uliyafanyia nini yale uliyojifunza?”

52 – Abul-Fath Hilaal bin Ja´far al-Haffaar ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Muhammad as-Swaffaar ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdil-Malik ad-Daqiyqiy ametukhabarisha: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Warqaa’ ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin ´Ubaydillaah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Enyi ummah! Mimi sichelei juu yenu kwa yale msiyoyajua, lakini tazameni ni vipi mnatendea kazi yale mliyojifunza.”[2]

53 – Abul-Fath Hilaal bin Ja´far al-Haffaar ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Muhammad as-Swaffaar ametukhabarisha: ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin Mansuur al-Haarithiy ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Hariyz bin ´Uthmaan ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy ´Awf, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:

”Hakika mambo yalivyo ni kwamba mimi naogopa kitu cha kwanza atachoniuliza Mola wangu: ”Ulijua; ni vipi uliyafanyia kazi yale uliyojifunza?”[3]

[1] Dhaifu mno. Haafidhw Ibn Hajar amesema kuwa Yahyaa bin ´Ubaydillaah at-Taymiy al-Madaniy ni mwenye kuachwa, ilihali al-Haakim amemtuhumu kutunga.

[2] Dhaifu mno.

[3] Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Ni kweli kwamba al-Haarithiy amezungumza kidogo, lakini inatiwa nguvu na cheni ya wapokezi inayofuatia.

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 39-41
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy