102 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ghundar ametukhabarisha, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Husayn, kutoka kwa Hilaal bin Yasaaf, ambaye amesema:
“Hakuna jambo gumu kwa muumini kama utakasifu wa nia yake.”
103 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Ziyaad ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´d, kutok kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Aliy bin al-Husayn, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Miongoni mwa Uislamu mzuri wa mtu ni kuacha yale yasiyomuhusu.”[1]
104 – Abu Bakr ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Idriys ametukhabarisha, kutoka kwa Ismaa´iyl, kutoka kwa Zubayr, ambaye ameeleza kuwa ´Abdullaah amesema:
“Zungumza kheri utatambulika kwayo, ifanyie kazi utakuwa miongoni mwa watu wake.”
105 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Daawuud bin Shaabuur, kutoka kwa Mujaahid, ambaye amesema:
“Luqmaan aliulizwa: “Kipi kilichokufikisha hapa?” Akasema: “Kumcha Allaah na kukaa kimya kwa muda mrefu.”
106 – al-Huutwiy ametukhabarisha: al-Waliyd bin Muslim ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd bin ´Abdil-´Aziyz, kutoka kwa al-Mashyakhah, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:
“Hakuna kheri katika maisha isipokuwa kwa watu wawili: mkimya mchaji, au mzungumzaji mwenye kupata faida.”
107 – Abu Bakr ametukhabarisha: Shabaabah ametukhabarisha, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Sayaar, ambaye amesema:
”Luqmaan aliulizwa: ”Umeifikiaje hekima yako?” Akasema: “Siulizi nisichohitaji na wala siulizi juu ya yale yasiyonihusu.”
108 – al-Huutwiy ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametukhabarisha: al-Mutw´im bin al-Muqdaam as-Swan´aaniy ametukhabarisha, kutoka kwa Naswiyh ash-Shaamiy, kutoka kwa Rakb al-Miswriy, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Pepo kwa yule mwenye kuifanyia kazi elimu yake, akatoa chenye kuzidi kutoka katika mali yake na akashikamana na kilichobaki kutoka katika neno lake.”[2]
109 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Misw´ar, kutoka kwa ´Atwaa’, ambaye amesema:
“Jihadharini na mkorogeko wa ndoto.”
110 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abul-Ahwasw ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abul-Mughiyrah, kutoka kwa Hudhayfah, ambaye amesema:
“Nilimshtakia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) maneno ya kipuuzi, akasema: “Uko wapi wewe na kuomba msamaha?”[3]
[1] at-Tirmidhiy (2318). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2318).
[2] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (3642).
[3] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah” (767).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 25-26
- Imechapishwa: 30/06/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 25-26
Imechapishwa: 30/06/2025
https://firqatunnajia.com/13-hekima-ya-luqmaan/