13. Hawa ndio walikuwa wajuzi zaidi wa tafsiri ya Qur-aan

Kuhusu tafsiri ya Qur-aan watu wenye ujuzi ni wa Makkah. Kwa sababu walikuwa ni maswahiba wa Ibn ‘Abbaas, kama vile Mujaahid, ‘Atwaa bin Abiy Rabbaah, ‘Ikrimah – aliyekuwa mjakazi wa Ibn ‘Abbaas – na wengineo kama vile Twaawuus, Abu ash-Sha’thaa’, Sa´iyd bin Jubayr na mfano wao. Vivyo hivyo watu wa Kuufah katika maswahiba wa Ibn Mas’uud, jambo ambalo liliwapambanua kutokana na wengine. Wanazuoni wa Madiynah katika tafsiri ya Qur-aan ikiwa ni pamoja na Zayd bin Aslam, ambaye Maalik na mwanaye ´Abdur-Rahmaan walisoma kwake tafsiri ya Qur-aan, kisha ‘Abdullaah bin Zayd, kisha baada ya hapo ´Abdullaah bin Wahb akasoma tafsiri ya Qur-aan kusoma ´Abdur-Rahmaan.

  • Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 54
  • Imechapishwa: 01/04/2025