13. Hadiyth “Waadilifu watakuwa juu ya mimbari za nuru… “

Hadiyth ya saba

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[1]

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

“Bali mikono Yake imekunjuliwa hutoa atakavyo.”[2]

يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ

”Mkono wa Allaah uko juu ya mikono yao.”[3]

61 – Abu Hafsw ´Umar bin ´Abdil-Mun´im al-Qawwaas ametukhabarish, kutoka kwa Abul-Yumn Zayd bin al-Hasan al-Muqriy’: Ismaa´iyl bin Ahmad al-Kutubiy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin an-Naqquur ametuhadithia: Muhammad bin Ahmad bin ´Imraan ametuhadithia: Abu Rawq al-Hamadhaaniy ametuhadithia: Ahmad bin Rawh ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa ´Amr bin Aws, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waadilifu watakuwa juu ya mimbari za nuru upande wa mkono wa kulia wa Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall) na mikono Yake yote ni ya kuume; wale wanaofanya uadilfu pale wanapohukumu, katika familia na katika walio chini yao.”[4]

Ameipokea Muslim.

Kuna Hadiyth nyingi mfano wa hizo ambazo haziwezi kupindishwa maana. Miongoni mwazo ni:

62 – Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah atazikunja mbingu siku ya Qiyaamah, kisha atazishika kwa mkono Wake wa kulia. Halafu atasema: “Mimi ndiye Mfalme! Halafu atazikunja ardhi saba, kisha atazishika kwa mkono Wake wa kushoto kisha atasema: “Mimi ndiye Mfalme! Wako wapi wenye jeuri? Wako wapi wenye kiburi?”[5]

63 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi mja anapotoa swadaqah katika vilivyo vizuri, basi Allaah huipokea na kuichukua kwa mkono Wake wa kuume na kisha akailea, kama ambavyo mmoja wenu anamlea mtoto wa ng´ombe, kama inakuwa kama Uhud. Mtu anapotoa swadaqah ya tonge, basi linakuwa mkononi mwa Allaah mpaka linakuwa kama Uhud. Kwa hivyo toeni swadaqah!”[6]

64 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkono wa kuume wa Allaah (´Azza wa Jall) umejaa. Haupungui kwa kutoa usiku na mchana. Katika mkono Wake mwingine kuna mizani ambayo anashusha na kupandishwa kwao.”[7]

65 –  al-Bukhaariy amepokea kwamba Ibn ´Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah atazishika ardhi kwa mkono Wake wa kushoto na mbingu zitakuwa kwenye mkono Wake wa kulia kisha aseme: “Mimi ndiye Mfalme.”[8]

Hadiyth zote hizi ni Swahiyh.

[1] 38:75

[2] 05:64

[3] 48:10

[4] Muslim (1827).

[5] al-Bukhaariy (7413) na Muslim (2148).

[6] ´Abdur-Razzaaq (20050).

[7] al-Bukhaariy (4684), Muslim (993), Ahmad (2/242) na at-Tirmidhiy (3045) ambaye amesema:

”Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh na inafasiri Aayah:

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

“Bali mikono Yake imekunjuliwa hutoa atakavyo.” (05:64)

Hadiyth imepokelewa na maimamu. Tunaiamini kama ilivyokuja pasi na tafsiri wala kuifanyia namna. Hivo ndivo walivosema maimamu wengi akiwemo Sufyaan ath-Thawriy, Maalik bin Anas, Ibn ´Uyaynah na Ibn-ul-Mubaarak; zinatakiwa kusimuliwa na kuaminiwa pasi na kuzifanyia namna.”

[8] al-Bukhaariy (7413).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 73-76
  • Imechapishwa: 03/06/2024