248- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Naapa kwa Allaah kwamba mimi namuomba Allaah msamaha na kutubia Kwake kwa siku moja zaidi ya mara sabini.”[1]
249- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Enyi watu! Tubuni kwa Allaah! Hakika mimi natubia Kwake kwa siku mara mia moja.”[2]
250- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote anayesema:
أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَىُّ الْقَيُّومُ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ؛ غُفِرَ لَهُ وَإِنْ كَانَ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ
”Namuomba msamaha Allaah, ambaye hapana mungu wa haki asiyekuwa Yeye, Aliyehai daima, anayekisimamia kila kitu, na natubia Kwake.”
basi Allaah atamsamehe ingawa ana dhambi ya kukimbia vitani.”[3]
251- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola Wake katika nusu ya mwisho wa usiku. Mkiweza kuwa miongoni mwa wale wanaomtaja Allaah katika saa hiyo, basi fanyeni hivo.”[4]
252- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mahali mja anapokuwa karibu zaidi na Mola Wake ni pale anapokuwa amesujudu. Hivyo ombeni du´aa kwa wingi.”[5]
253- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Wakati mwingine moyo wangu hughafilika na mimi humuomba Allaah msamaha kwa siku mara mia moja.”[6]
[1] al-Bukhaariy katika al-Fath (11/101).
[2] Muslim (04/2076).
[3] Abu Daawuud (02/85), at-Tirmidhiy (05/569) na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahaby (01/511) akaafikiana naye. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy. Tazama ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/182) na ”Jaamiy’-ul-Usuwl-il-Ahaadiyth ar-Rasuul (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)” (04/389-390) kwa ukaguzi wa al-Arnaauutw.
[4] at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy (01/279) na al-Haakim. Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/183) na “Jaamiy’-ul-Usuwl” kwa ukaguzi wa al-Arnaauutw (04/144).
[5] Muslim (01/350).
[6] Muslim (04/2075). Ibn-ul-Athiyr amesema: ”Ni kufunikwa kwa moyo.” Lakini kilichokusudiwa hapa ni usahaulifu. Kwa sababu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa siku zote ni mwenye kufanya Dhikr kwa wingi, kujikurubisha kwa Mola wake na kudumu katika hali ya kujua kuwa Allaah anamchunga. Basi baadhi ya nyakati pale anaposahau kitu katika hayo au akasahaulishwa, basi huzingatia kuwa ni dhambi juu ya nafsi yake. Hivyo hukimbilia katika kuomba msamaha.” Tazama ”Jaamiy´-ul-Usuwl” (04/386).
- Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huswn-ul-Muslim
- Imechapishwa: 09/05/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)