al-Qummiy al-Baatwiniy amesema wakati alipokuwa akifasiri maneno Yake (Ta´ala):
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا
“Vivyo hivo tumemfanyia kila Nabii maadui mashaytwaan wa kiwatu na kijini – wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba – kwa udanganyifu.”[1]
“Bi maana Allaah hakumtuma Mtume yeyote isipokuwa katika Ummah wake walikuwepo mashaytwaan wa kijini na wa kibinaadamu. Wakiambizana wao kwa wao kwamba wasiamini maneno ya kupambapamba, kwa sababu Wahy huu ni uongo.”
Halafu akasimulia kwamba Abu ´Abdillaah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Allaah hakumtuma Mtume isipokuwa katika Ummah wake walikuwepo mashaytwaan wawili ambao wanamuudhi na kuwapotosha watu baada yake. Kuhusu watu wa Nuuh alikuwa ni Qantwifuusw na Khiraam, watu wa Ibraahiym alikuwa ni Paulo na Mariytuun na watu wa Muhammad alikuwa ni Habtar na Zurayq.”
Kamwe Abu ´Abdillaah asingelisema uongo huu! Hakuwa anajua mambo yaliyofichikana. Haya si mengine isipokuwa ni Wahy wa shaytwaan wa ma-Raafidhwah na Baatwiniyyah ili waweze kufikia kuwatukana Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tazama Aayah hii jinsi inavyowataja maadui wa Mitume kwa njia ya wingi:

“Vivyo hivo tumemfanyia kila Nabii maadui mashaytwaan wa kiwatu na kijini – wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba – kwa udanganyifu.”
Lakini ili Baatwiniy huyu aweze kuzimwaga chuki zake kwa Abu Bakr na ´Umar anamzulia kila Mtume kuwa na maadui wawili. Kisha akamvamilia Abu Bakr na ´Umar kwa kusema:
“… na watu wa Muhammad alikuwa ni Habtar na Zurayq.”
Akimaanisha Abu Bakr na ´Umar. Kwa nini? Kwa sababu walitokomeza ukafiri uliokuwa ukiongozwa na mababu wa Raafidhwah na Baatwiniyyah Musaylamah al-Kadhdhaab na al-Aswad al-´Ansiy na vilevile waliweka msingi kuanguka kwa utawala wa mababu zao, marafiki zao na mabwana zao, utawala wa kiajemi na warumi.
[1] 06:112
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 186-187
- Imechapishwa: 20/06/2018

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 186-187
Imechapishwa: 20/06/2018
https://firqatunnajia.com/129-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-tisa-wa-al-anaam/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)