Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
103 – Hatuoni kuwa imeumbwa na wala hatuendi kinyume na mkusanyiko wa waislamu.
MAELEZO
Hatusemi kuwa Qur-aan imeumbwa tofauti na wanavosema Jahmiyyah. ´Aqiydah hiyo ni ukafiri na kupinga maneno ya Allaah. Aidha ni kumsifu Allaah mapungufu na kumtuhumu kuwa hazungumzi. Ambaye hazungumzi anakuwa mpungufu, hawezi kuwa Mungu, Msamaria alisema kuhusu ile sanamu ya ndama iliyochongwa:
هَـٰذَا إِلَـٰهُكُمْ وَإِلَـٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ
“Huyu ndiye mwabudiwa wenu na mwabudiwa wa Muusa lakini amesahau.”[1]
Ndipo Allaah (Jalla wa ´Alaa) akasema:
أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا وَلَا يَمْلِكُ لَهُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا
“Je, hawaoni kwamba [ndama huyo] harejeshi neno na wala hawezi kuwadhuru na wala kuwanufaisha?”[2]
Bi maana hazumgumzi. Kwa hivyo ikathibitisha juu ya ubatili wa kumwabudu. Katika Aayah nyingine imekuja:
أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا
“Je, hawakuona kuwa huyo [ndama] hawazungumzishi na wala hawaongozi njia?”[3]
Maneno ni sifa ya ukamilifu na kutozungumza ni sifa ya upungufu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametakasika kutokamana na sifa za mapungufu na anasifiwa kwa sifa kamilifu.
Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:
”… na wala hatuendi kinyume na mkusanyiko wa waislamu.”
Mkusanyiko wa waislamu wanaamini kuwa Qur-aan imeteremshwa kutoka kwa Allaah na si kiumbe. Qur-aan imeanza kutokana na Allaah na Kwake ndio itarudi. Hii ndio ´Aqiydah ya waislamu juu ya Qur-aan. Hatuenda kinyume na ´Aqiydah ya waislamu katika yale yote waliyokubaliana:
وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا
”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!”[4]
Qur-aan imeanza kutoka kwa Allaah, na si kama wanavosema baadhi ya wapotofu, ya kwamba Jibriyl aliichukua Qur-aan kutoka katika Ubao uliohifadhiwa. Jibriyl aliisikia moja kwa moja kutoka kwa Allaah. Baada ya hapo Qur-aan itarudi kwa Allaah, bi maana katika zama za mwisho. Hiyo ni miongoni mwa alama za Qiyaamah. Qur-aan itaondolewa kutoka katika misahafu na vifua vya watu na hivyo haitokuweko tena ardhini.
[1]20:88
[2]20:89
[3]7:148
[4]4:115
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 137
- Imechapishwa: 13/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket