al-Qummiy amesema katika mnasaba wa Aayah:
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ
“Nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Allaah uongi au akasema: “Nimefunuliwa Wahy”, na hali hakufunuliwa Wahy wowote na yule aliyesema: “Nitateremsha mfano wa yale aliyoyateremsha Allaah? Lau ungeliwaona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti na Malaika wamenyosha mikono yao [kuwaelekezea wakisema]: “Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki na mlikuwa mkitakabari kuhusu Aayah Zake.”[1]
“Yeye (´Azza wa Jall) anaeleza yale yanayowakuta maadui wa familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa kufa na akasema:
وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ
“Lau ungeliwaona madhalimu… “
Bi maana wale waliowapokonya kizazi cha Muhammad haki yao:
فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ
“… pale wakiwa katika mateso makali ya mauti na Malaika wamenyosha mikono yao [kuwaelekezea wakisema]: “Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha… “
Bi maana kiu:
بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ
“… kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki na mlikuwa mkitakabari kuhusu Aayah Zake.”[2]
“Bi maana walikanusha yale yaliyoteremshwa juu ya familia ya Muhammad.”
Madhalimu hapa ni makafiri washirikina na yale yanayowakuta wakati wa kufa. Raafidhwah hawajali kufuru na shirki. Ni kama kwamba makafiri washirikina hawastahiki adhabu hii iliyotajwa. Kwa ajili hiyo ndio maana wanapindisha yale yote yanayowahusu makafiri na wanafiki kwenda kwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wote wanaofuata mfumo wao. Madai yao ni kwamba wamewadhulumu familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wamewapokonya haki ya familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wamepinga uongozi wa maimamu na wasii wao. Wamefanya uongo huu ni wenye kupinzana na Qur-aan tukufu.
Sidhani hata kama mayahudi na manaswara wamefikia kiwango hichi katika kuwa na ujasiri wa kukikengeusha Kitabu cha Allaah. Allaah hakuteremsha Aayah hata moja kuhusu uongozo wa kizazi cha Muhammad. Maswahabah wa Muhammad hawakukanusha chochote kuhusu kizazi cha Muhammad. Walikuwa wakiwatukuza na wakiwapenda.
Baatwiniyyah hawa wamefanya haki ya maimamu wao kuwa kubwa kuliko haki ya Allaah kwa njia ya kipekee. Kutokana na hilo wamepotosha Aayah zote zinazohusiana na kuabudiwa kwa Allaah pekee na haki nyenginezo za Allaah kwenda katika uongozi na uimamu na vilevile wamekengeusha Aayah zinazohusu Qiyaamah, kufufuliwa na malipo kwenda kwa Mahdiy wao aliyezuliwa na wamewapa maimamu nafasi ya juu zaidi kuliko Mitume.
[1] 06:93
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/211).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 184-185
- Imechapishwa: 17/06/2018

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 184-185
Imechapishwa: 17/06/2018
https://firqatunnajia.com/127-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-saba-wa-al-anaam/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)