243- Weka mkono wako katika kile kiungo kinachokuuma katika mwili wako kisha useme:
بِسْمِ الله
“Kwa jina la Allaah.”
mara tatu. Kisha useme:
أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ
“Najilinda kwa Allaah na kwa uwezo Wake kutokamana na shari ya ninachokihisi na ninachokitahadhari nacho.”[1]
[1] Muslim (03/1728).
- Muhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huswn-ul-Muslim
- Imechapishwa: 09/05/2020