122. Huko ndio inatoka dini yetu – ni wapi inatoka dini yao?

Salaam (afk. 171), msomaji wa Baswrah.

145 – ´Affaan bin Muslim amesema:

”Nilikuwa kwa Salaam Abul-Mundhir, msomaji wa watu wa Baswrah, wakati alipojiliwa na bwana mmoja akiwa na msahafu na akasema: ”Je, hii si inayo makaratasi na mafuta na hivyo ni kiumbe?” Salaam akamwambia bwana yule: ”Inuka, zandiki.”[1]

Qaadhiy Shaariyk (afk. 177 au 178), mmoja katika wanazuoni wakubwa.

146 – ´Abbaad bin al-´Awwaam amesema:

”Miaka khamsini iliyopita Shariyk bin ´Abdillaah alitujilia. Nikasema: “Ee Abu ´Abdillaah! Sisi tuko na watu katika Mu´tazilah ambao wanazipinga Hadiyth hizi:

“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) kila usiku hushuka katika  mbingu ya dunia.”

na:

“Watu wa Peponi watamuona Mola wao.”

hivyo Shariyk akanihadithia karibu Hadiyth kumi juu ya hili. Kisha akasema: “Ama sisi tumeichukua dini yetu kutoka kwa wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa Maswahabah wameichukua kutoka kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wao wameichukua dini yao kutoka kwa yupi?”[2]

[1] Mtunzi amemsimulia kupitia kwa Abu Haatim ar-Raaziy: Ya´quub bin Yuusuf bin al-Jaaruud amenihadithia, kutoka kwa ´Affaan bin Muslim. Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kutoka kwa Salaam. ´Affaan alikuwa ni mwenye kuaminika na alikuwa ni katika wanaume wa al-Bukhaariy na Muslim. Ibn Abiy Haatim amesema kuhusu Ya´quub bin Yuusuf ad-Dashtakiy:

”Baba yangu amepokea kutoka kwake na akaulizwa juu yake, ambapo akajibu kuwa ni mkweli.”  (al-Jarh wat-Ta´diyl (4/2/217))

[2] Ameitaja kupitia kwa Muhammad bin Ishaaq as-Swaaghaaniy: Silm bin Qaadim ametuhadithia: Muusa bin Daawuud ametuhadithia: ´Abbaad bin al-´Awwaam ametuhadithia. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na wapokezi wote ni wenye kuaminika na ni wanaume wa Muslim – isipokuwa Silm bin Qaadim, ambaye alikuwa ni mwenye kuaminika kwa mujibu wa al-Khatwiyb katika “Taariykh Baghdaad” (9/145). Elimu hii haikutajwa katika ”al-Lisaan” na kwa ajili hiyo imeambatanishwa nayo. Ibn Mandah ameipokea katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd” (01/97 – muswada) kupitia njia zingine, kutoka kwa al-´Abbaad, kwa upokezi mfano wake unaosema:

”Ni kipi wanachopinga? Wale waliofikisha swalah na mambo yanayopendeza kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio haohao waliofikisha mambo haya.”

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh pia.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 144-145
  • Imechapishwa: 21/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy