120. Dalili ya kwanza kufaa kwa mwanamke kuyatembelea makaburi

116 – Wanawake ni sawa na wanaume katika  mapendekezo ya kuyatembelea makaburi. Hilo ni kwa sababu zifuatazo:

1 – Kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”… yatembeleeni makaburi.”

Hivyo wanawake pia wanaingia humo. Ubainifu wake ni kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokataza kutembelea makaburi mwanzoni, hapana shaka kwamba alikataza kwa jinsia zote mbili, wanaume na wanawake. Kwa hivyo pindi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Nilikuwa nimewakatazeni kuyatembelea makaburi.”

ina maana kwamba alikuwa anamaanisha jinsia zote, kwani alikuwa anawaelezea yale aliyoyakataza hapo awali. Kwa hivyo mambo yakishakuwa namna hiyo basi maana yake ni kwamba wanaozungumzishwa katika sentesi ya pili isemayo:

”… yatembeleeni… ”

yanajumuisha jinsia zote mbili. Kitu kinachotilia nguvu mtazamo huo ni kwamba mantiki ya mazungumzo ya Hadiyth ya Muslim kuhusu Hadiyth ya Buraydah iliyotajwa awali:

”Nilikukatazeni kuhusu kula nyama za Udhhiyah zaidi ya siku tatu, basi kaeni nazo kadiri mnavyotaka. Nilikukatazeni kuhusu kunywa kinywaji kilichochachishwa isipokuwa katika viriba, basi kunyweni katika vyombo vyote lakini msinywe kilevi.”

Mazungumzo haya yote hapana shaka kwamba yalikuwa yameelekezwa kwa jinsia zote mbili, kama mambo yalivyo katika mazungumzisho ya kwanza:

”Nilikuwa nimewakatazeni… ”

Basi mtu akisema kwamba mazungumzisho katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”… yatembeleeni… ”

yanawahusu wanaume pekee, linavuruga ufasaha wa maneno, jambo ambalo haliwezekani kwa yule ambaye amepewa mkusanyiko wa maneno mafupi yenye maana pana na ambaye ni mfasaha zaidi kati ya waliotamka kwa lugha ya kiarabu – swalah na amani zimwendee yeye. Hilo linatiliwa nguvu na sababu zifuatazo:

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 229
  • Imechapishwa: 04/08/2026