al-Qummiy amesema:
“Ja´far bin Ahmad ametuhadithia: ´Abdul-Kariym ametuhadithia: Muhammad bin ´Aliy ametuhadithia: Muhammad bin al-Fudhwayl ametuhadithia, kutoka kwa Abu Hamzah ambaye ameeleza ya kwamba alimuuliza Abu Ja´far kuhusiana na maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
“Wale ambao wamekadhibisha Aayah Zetu ni viziwi na mabubu katika viza. Allaah humpotoa amtakaye na humuweka amtakaye katika njia iliyonyooka.”[1]
Akajibu: “Imeteremshwa kuhusu wale waliowakadhibisha wausiwa. Ni visiwi na mabubu gizani, kama alivyosema Allaah. Yule ambaye ni miongoni mwa wana wa Ibliys hawasadikishi wausiwa wala hawaamini. Hao ndio wale ambao Allaah amewapoteza. Kuhusu wale ambao ni katika wana wa Aadam wanawaamini wausiwa.”[2]
Allaah amemtakasa Abu Ja´far kutokamana na uongo huu na kuzipotosha Aayah za Allaah. Baatwiniyyah huyu malengo yake hapa ni kuwakufurisha Maswahabah na waislamu wengine wote.
Jengine ni kwamba Aayah imeteremshwa Makkah, kabla ya kuzaliwa kwa wale wanaoitwa wausiwa na kabla ya hata ´Aliy kumuuoa Faatwimah. Enyi waongo! Ni lini yalikuwa makadhibisho haya ambayo Allaah ameyateremshia Aayah za Qur-aan! Malengo ya Takfiyr hii ni kwa Maswahabah ambao wako gizani ilihali Raafidhwah, wafuasi wa Ibn Sabaa´ myahudi, wao wako katika njia iliyonyooka.
Katika uongo huu kuna matusi kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ujumbe wake. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
الر ۚ كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ
“Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu kutoka katika viza na kuwapeleka katika nuru kwa idhini ya Mola wao, waelekee katika njia ya Mwenye nguvu kabisa, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”[3]
Amesema (Ta´ala) akiwazungumzisha Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا
“Yeye ndiye anakurehemuni na Malaika Wake wanakuombeeni ili akutoeni kutoka katika viza kwenda katika nuru; Naye ni Mwenye kuwarehemu waumini.”[4]
Ninaapa kwa Allaah ya kwamba aliwatoa katika viza vya ukafiri na shirki, kama alivyoahidi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) – na Yeye si mwenye kwenda kinyume na ahadi Zake. Rehema za Allaah zimewafikia. Lakini Raafidhwah Baatwiniyyah madhalimu hakuna jengine wanachotaka isipokuwa ni kumkadhibisha Allaah. Hakuna jengine wanachotaka Raafidhwah Baatwiniyyah isipokuwa kukufuru Aayah hizi. Bila shaka wao ndio ambao wanazama katika viza na upotevu.
[1] 06:39
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/199).
[3] 14:01
[4] 33:43
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 177-178
- Imechapishwa: 02/06/2018

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 177-178
Imechapishwa: 02/06/2018
https://firqatunnajia.com/120-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-tatu-wa-al-anaam/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)