12. Swalah ndani ya msikiti ulio na kaburi

Swali 12: Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya msikiti ikiwa ndani yake kuna kaburi, katika kiwanja chake au upande wa Qiblah chake?

Jibu: Ikiwa ndani ya msikiti kuna kaburi basi kuswali ndani yake si sahihi. Ni mamoja liko mbele ya waswaliji, upande wao wa kulia au upande wao wa kushoto. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah awalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni mahali pa kuswalia.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tanabahini! Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa mahali pa kuswalia. Tanabahini! Msiyafanye makaburi kuwa mahali pa kuswalia. Hakika mimi nawakatazeni na hilo.”

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Isitoshe kuswali kwa kulielekea kaburi ni miongoni mwa njia za shirki na kuchupa mpaka kwa waliyomo ndani ya makaburi. Kwa hivyo ikalazimika kukataza jambo hilo kwa ajili ya kutendea kazi Hadiyth mbili zilizotajwa na nyinginezo zilizopokelewa zikiwa na maana kama hiyo na kadhalika kwa ajili ya kuzuia njia zinazopelekea katika shirki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 11/08/2022