Hajj yenye kukubaliwa ina sifa zifuatazo:

1 – Kuwa matumizi yote ni kutoka katika mali halali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah ni Mzuri na wala hakubali isipokuwa kilicho kizuri…”[1]

Ameipokea Muslim.

2 – Kumtakasia matendo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kufuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

3 – Kujiepusha kabisa na maasi na madhambi, pamoja na Bid´ah na mambo yanayoenda kinyume na Shari´ah.

4 – Tabia njema, unyenyekevu, huruma kwa wengine na kutojikweza katika mavazi au kipando, katika kutangamana na watu wengine, kama alivyokuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hajj yake. Ibn ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hajj yenye kukubaliwa ni ile isiyokuwa kujionyesha, kutaka kusikika, matusi na jimaa wala ufuska na ifanywe kwa mali halali…”[2]

[1] Ameipokea Muslim (1015).

[2] at-Tamhiyd (22/39).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 18
  • Imechapishwa: 11/05/2025