Kwa hivyo ni lazima kwa anayejinasibisha na Salaf ahakikishe jina hilo na kujinasibisha kwa njia ya kwamba awakilishe mfumo wa Salaf inapokuja katika ´Aqiydah, maneno, vitendo na matangamano yake ili awe Salaf wa kweli na awe kiigizo chema ambaye anawakilisha mfumo wa Salaf.

Kwa hivyo yeyote anayetaka mfumo huu basi analazimika kuutambua na kuusoma. Kwanza yeye aujue, aulinganie na awabainishie watu. Hii ndio njia ya uokovu na ndio mfumo wa kundi lililookoka; Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni wale wanaofuata mfano wa yale aliyokuwa akifuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, akasubiri na kuwa imara juu ya hayo na asipelekwe na mitihani, propaganda zinazopotosha na asitikiswe na vimbunga. Bali anakuwa imara juu ya yale aliyomo mpaka pale atapokutana na Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah awawafikishe wote katika yale anayoyapenda na kuyaridhia.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah zake wote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Salafiyyah haqiyqatuhaa wa simaatuhaa, uk. 38-40
  • Imechapishwa: 06/05/2024