48 – Muhammad bin Abiy ´Aliy al-Aswbahaaniy alitusomea mashairi:

Ee mwanaume! Ifanyie kazi elimu yako utashinda

Elimu hainufaishi kitu bila ya matendo mema

Elimu ni pambo na kumcha Allaah ndio pambo lake

Wale wanaomcha Allaah wanajishughulisha na elimu

Ee mwenye elimu! Hoja ya Allaah ni yenye kushinda!

Si vitimbi wala hila zinanufaisha dhidi yake

Jifunze elimu na uifanyie kazi vile unavyoweza

Usiache upuuzi na mabishano yakakushughulisha kuitafuta kwake

Wafunze watu na ukusudie kuwanufaisha

Na tahadhari kwelikweli usichoke

Muwaidhi ndugu yako kwa upole kutokana na kosa lake,

kwa sababu yule aliyefungana na elimu hutumbukia kwenye kosa

Unapokuwa kati ya watu walionyimwa

basi waamrishe mema ikiwa hawajui

Wasipokutii warejelee bila kukereka

Subiri na uvute subira na usihuzunike kwa wanayoyafanya

Kila mwana-kondoo amesimamishwa kwa miguu yake na ikiwa

watashikilia dhuluma  na kudhulumu basi jiweke kivyako

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy