12. Je, inasihi kuswali nyuma ya imamu anayewaomba msaada wafu na kuwataka msaada wao?

Swali 12: Je, inasihi kuswali nyuma ya imamu anayewaomba msaada wafu na kuwataka msaada wao?

Jibu: Mtu huyu ni kafiri. Yule anayewaomba msaada wafu, kuwataka msaada wao, kuwaomba watimize mahitaji yake na wamuondolee majanga, basi huyu ni mshirikina. Swalah haisihi nyuma yake na swalah nyuma yake ni batili. Na mwenye kuswali nyuma yake bila kujua hali yake, kisha baadaye akajua, basi anatakiwa kurudia swalah yake. Hili ni kwa mujibu wa maafikiano ya waislamu kwamba swalah haisihi nyuma ya mshirikina. Hata hivyo kuna tofauti ya maoni miongoni mwa wanazuoni kuhusu kuswali nyuma ya fasiki. Madhehebu ya Hanaanabilah na wengineo wanakataza kuswali nyuma yake na wanaona kuwa haisihi. Wengine wanaona kuwa inasihi licha ya kwamba inachukiza kufanya hivo. Maoni sahihi ni kwamba inasihi ingawa bora zaidi kuswali nyuma ya mtu mwadilifu. Hapa ni pale ambapo atakuwa mpwekeshaji lakini hata hivyo ni fasiki. Ama akiwa ni mshirikina, basi haisihi kuswali nyuma yake kwa maafikino.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 31
  • Imechapishwa: 06/01/2026