Ni jambo linalofahamika kwamba nukuu katika tafsiri ya Qur-aan kwa kiasi kikubwa yanafanana na yaliyonakiliwa juu ya masuala ya vita na magomvi. Kwa sababu hiyo Imaam Ahmad amesema:
“Kuna mambo matatu hayana cheni ya wapokezi: Tafsiri ya Qur-aan, masimulizi ya magomvi na ya vita.”
Kuna upokezi mwingine unaosema kuwa hayana msingi, kwa maana cheni ya wapokezi. Kwa sababu mengi yao yanategemea masimulizi yasiyo na mfululizo kamili wa wapokezi, kama yale yanayosimuliwa ‘Urwah bin az-Zubayr, ash-Sha’biy, al-Zuhriy, Muusa bin ‘Uqbah, Ibn Ishaaq na wale waliokuja baada yao kama vile Yahyaa bin Sa’iyd al-Umawiy, al-Waliyd bin Muslim, al-Waqiydiy na mfano wao katika masimulizi ya vita. Hakika watu wajuzi zaidi wa masuala ya vita ni watu wa Madiyna, kisha watu wa Shaam halafu watu wa ´Iraaq. Watu wa Madiyna walikuwa na ujuzi zaidi wa jambo hilo kwa sababu vilitokea kwao. Watu wa Shaam walikuwa ni watu wa vita na jihaad, hivyo walikuwa na elimu juu ya jihaad na masimulizi ya matukio ya kihistoria ambayo wengine hawakuwa nayo. Kwa sababu hiyo watu walikitukuza sana kitabu cha Abu Ishaaq al-Fazariy alichokiandika kuhusu masuala haya na pia walimzingaia al-Awzaa´iy kuwa ndiye mwenye ujuzi zaidi katika mlango huu wa masimulizi ya vita miongoni mwa wanazuoni wa miji mbalimbali.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 52-54
- Imechapishwa: 01/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)