Daku ina faida nyingi ikiwa ni pamoja na:

1 – Kutekeleza amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2 – Daku inayo baraka. Kwa hiyo mfungaji anatarajia baraka hii iliyobainishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

3 – Kwenda kinyume na watu wa Kitabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kipambanuzi kati ya swawm yetu na swawm ya watu wa Kitabu ni kula daku.”[1]

4 – Allaah anamsifu na Malaika Wake wanawaombea du´aa wanaokula daku. Abu Sa’iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Daku ni chakula chenye baraka, basi msikikose ijapo kwa kunywa funda moja ya maji. Kwa hakika Allaah anamsifu na Malaika Wake wanawaombea du´aa wale wanaokula daku.”[2]

5 – Kunampa nguvu mfungaji ya kufanya ´ibaadah.

Licha ya fadhilah hizi zote bado baadhi ya watu hula mlo katikati ya usiku, kisha wanalala na hukosa fadhilah hizi. Na huenda asiamke mpaka baada ya jua kuchomoza na basi haswali isipokuwa baada ya jua kuchomoza kwa makusudi na ikawa hilo ndilo tabia yake daima. Kwa hivyo atakuwa amefanya jinai kubwa zaidi kuliko jinai ya mzinifu, mwizi, mnywaji wa pombe na mwenye kuwakosea wazazi wake. Hadi baadhi ya wanazuoni walitoa fatwa kuwa ni mwenye kuritadi – na ulinzi unaombwa kutoka kwa Allaah – ikiwa alikuwa anakusudia hilo na ikawa ndiyo kawaida yake daima na hawi makini kufanya njia za kumsaidia kuamka kwa ajili ya swalah na wala hafanyi sababu za kumuwezesha kuamka kwa kuswali, bali hujizatiti tu kwa ajili ya kazi yake na hivyo anaitanguliza kazi badala ya swalah. Hivyo basi anakuwa ni mtu anayeipoteza swalah kwa makusudi ambayo ndiyo nguzo ya pili ya Uislamu. Na hata akidumu katika kufunga, basi funga yake haitamnufaisha kitu muda wa kuwa haswali[3].

[1] Muslim (1096).

[2] Ahmad (1006). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan (3467).

[3] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/374) ya Ibn Baaz.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/440-441)
  • Imechapishwa: 23/02/2025