72 – Abu Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kusoma usiku Aayah mbili mwishoni mwa Suurah al-Baqarah zitamtosheleza.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… zitamtosheleza.”

Bi maana zitamtosheleza kutokana na kila baya. Imesemekana pia kuwa zitamtosheleza kutokana na kisimamo cha usiku, ingawa maoni ya kwanza ndio bora zaidi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizisoma na akisimama usiku kuswali.

[1] al-Bukhaariy (5009) na Muslim (708).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 79
  • Imechapishwa: 26/10/2025