Hakuna yeyote anayejua maumbile ya Malaika isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na maumbile yao yanatofautiana na maumbile ya wanadamu:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۚ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Himdi zote ni stahiki ya Allaah muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mwenye kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbilimbili, tatutatu na nnenne. Huzidisha katika uumbaji Atakavyo – Hakika Allaah juu ya kila jambo ni Muweza.”[1]

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Jibriyl akiwa na mbawa 600 na kila mbawa inafunika upeo wa macho[2]. Kwa hivyo hakuna yeyote anayejua maumbile yao wala namna walivyo isipokuwa Allaah pekee. Watu hawawezi kumuona Malaika wakiwa na maumbile yao ya kihakika. Badala yake wanaweza kuwaona Malaika wakiwa katika maumbile ya mtu. Ni kama ambavyo Jibriyl alikuwa akimjilia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika maumbile ya mwanadamu na kukaa naye na kumzungumzisha. Mtume alimuona Jibriyl (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam) katika maumbile yake ya kihakika mara mbili: mara ya kwanza alimuona Makkah akiwa katika upeo wa macho na mara ya pili alimuona katika mkunazi usiku wa safari ya kupandishwa mbinguni. Mbali na mara mbili hizi Mtume alikuwa akimuona Jibriyl (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam) katika maumbile ya mwanadamu. Mara nyingi alikuwa akimjilia katika sura ya Dihyah al-Kalbiy (Radhiya Allaahu ´anh).

[1]35:1

[2] al-Bukhaariy (3232) na Muslim (174).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 129
  • Imechapishwa: 12/11/2024