119. al-Qummiy upotoshaji wake wa pili wa al-An´aam

al-Qummiy amesema:

“al-Husayn bin Muhammad bin al-Mu´laa bin Muhammad ametukhabarisha, kutoka kwa ´Aliy bin Asbaatw, kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Abu Baswiyr, kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake:

وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ

“Tunaapa kwa Allaah, ee Mola wetu, hatukuwa washirikina.”[1]

“Bi maana kuhusiana na uongozi wa ´Aliy.”[2]

Aayah hii ni miongoni mwa Aayah zengine ambazo zinawahusu makafiri washirikina ambao waliwakadhibisha Mitume watukufu na wakakadhibisha yale waliyokuja nayo katika Tawhiyd na wakamfanyia Allaah washirika ambao wanawaabudu badala ya Allaah. Allaah atawakemea kwa hilo na kuwauliza kuhusu waungu wao ambao walikuwa wakidai kuwa ni washirika pamoja na Allaah na wakidai kwamba eti hawakuwa washirikina. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ

“Nani mdhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Allaah uongo au anayekadhibisha Aayah Zake? Hakika madhalimu hawatofaulu! Siku Tutakayowakusanya wote pamoja kisha tutawaambia wale walioshirikisha: “Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mkidai?” Hapo haitokuwa fitina yao isipokuwa kusema: “Tunaapa kwa Allaah, ee Mola wetu, hatukuwa washirikina.”[3]

Baatwiniyyah wakaja kuzipotosha na kuzipindisha kwa maana ambayo haikutajwa si katika Qur-aan wala Sunnah. Si jengine isipokuwa ni uzushi na njama za myahudi Ibn Sabaa´ dhidi ya Uislamu. Hakuna walichofanya isipokuwa kuwafurahisha maadui wa Uislamu Baatwiniyyah. Nusu ya Qur-aan nzima imepindishwa kwa njia kama hii iliyozuliwa. Wamemkafirisha kila yule asiyeamini tafsiri hizi. Wanaonelea kuwa uongozi una daraja moja sawa na shahaadah ambapo yule asiyeuamini basi amemshirikisha Allaah. Kwa mujibu wao uongozi ni nguzo kubwa kabisa na ya muhimu; yule asiyeuamini basi amekufuru na kushirikisha.

Hawakutilia umuhimu mkubwa nyujumbe, kukiwemo ujumbe mkubwa wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama walivyotilia umuhimu mkubwa uongozi huu uliozuliwa. Bali ukilinganisha na uongozi ni jambo jepesi mno. Allaah amesema kweli juu yao pale aliposema (Ta´ala):

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ

“Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Allaah uongo au amekadhibisha Aayah Zake? Hakika wahalifu hawatofaulu.”[4]

Hakuna yeyote anayemsemea uongo Allaah kama wanavofanya watu hawa!

[1] 06:23

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/199).

[3] 06:21-24

[4] 10:17

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 176-177
  • Imechapishwa: 02/06/2018