5 – Yale anayoyaacha mtu kama athari njema na swadaqah yenye kuendelea. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala)
وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
”… na tunaandika yale waliyoyatanguliza na athari zao.”[1]
Vilevile kuna Hadiyth kuhusu hilo:
1 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapokufa mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema anayemuombea du´aa.”
Ameipokea Muslim (5/73) ambaye tamko ni lake, al-Bukhaariy katika ”al-Adab al-Mufrad”, uk. 8, Abu Daawuud (2/15), an-Nasaa’iy (2/129), at-Twahaawiy katika ”al-Mushkil” (1/85), al-Bayhaqiy (6/278) na Ahmad (2/372). Ziada ni kutoka kwa Abu Daawuud na al-Bayhaqiy.
2 – Abu Qataadah ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Bora ya yale anayoyaacha mtu baada yake ni matatu; mtoto mwema anayemuombea du´aa, swadaqah inayoendelea ambayo thawabu yake inamfikia na elimu inayofanyiwa kazi baada yake.”
Ameipokea Ibn Maajah (1/106), Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” (nr. 84-85), at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam as-Swaghiyr”, uk. 79, Ibn ‘Abdil-Barr katika ”Jaamiy’ Bayaan-il-‘Ilm” (1/15). Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh, kama alivyosema al-Mundhiriy katika ”at-Targhiyb” (1/58).
3 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) pia ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika katika yale yanayomfikia muumini miongoni mwa matendo na mema yake baada ya kufa kwake ni elimu aliyoifundisha na akaieneza, mtoto mwema aliyemwacha, msahafu alioacha kama urithi, msikiti alioujenga, nyumba aliyojenga kwa ajili ya wapita njia, mto aliouanzisha au swadaqah aliyoitoa kutoka katika mali yake wakati wa afya na uhai wake ambayo inamfikia baada ya kufa kwake.”
Ameipokea Ibn Maajah (1/106) kwa cheni ya wapokezi nzuri. Vilevile ameipokea Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” yake na al-Bayhaqiy, kama alivosema al-Mundhiriy.
4 – Jariyr bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Tulikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katikati ya mchana. Tahamaki wakaja watu wakiwa peku, uchi na wamevaa vitenge vya manyoya au mavazi ya ngozi ya ngamia, wamebeba mapanga [hawakuwa na kikoi wala kitu kingine zaidi ya hivyo]. Wengi wao ni kutoka Mudhwar, bali wote ni kutoka Mudhwar. Basi ukapiga wekundu… ”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”… ukatibadilika – (na maana zote mbili ni moja) uso wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoona hali yao ya umasikini walionayo. Akaingia, kisha akatoka, akamwamrisha Bilaal aadhini, kisha akaswali [Dhuhr, kisha akapanda juu ya mimbari ndogo], kisha akatoa Khutbah [akamhimidi na kumsifu Allaah] ambapo akasema:
”Ama baada ya hayo; hakika Allaah ameteremsha ndani ya Kitabu Chake:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا
“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni kutokana na nafsi moja na akaumba kutoka humo mke wake na akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Allaah ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah amekuwa juu yenu ni Mwenye kuchunga.”[2]
Pia Aayah ya ”al-Hashr”:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۚ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ
“Enyi walioamini! Mcheni Allaah na nafsi itazame nini imetanguliza kwa ajili ya kesho, na mcheni Allaah, kwani hakika Allaah ni Mjuzi wa khabari za dhahiri na siri juu ya yale myatendayo. Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah ambapo Naye Akawasahaulisha nafsi zao – hao ndio mafasiki. Hawalingani sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi, watu wa Peponi ndio wenye kufuzu.”[3]
”Toeni swadaqah kabla ya kuwekewa kizuizi baina yenu na swadaqah.”] Mtu atoe swadaqah kutoka katika dinari yake, kutoka katika dirhamu yake, kutoka katika nguo yake, kutoka katika pishi ya ngano yake, [kutoka katika shayiri yake], kutoka katika pishi ya tende yake, mpaka akafikia kusema:
”Wala asidharau yeyote miongoni mwenu kitu kidogo katika swadaqah, ijapo ni nusu ya tende.” [lakini watu walichelewa mpaka uso wake ukaonekana kuwa na ghadhabu]. Tahamaki akaja bwana mmoja anayetokana na Answaar na mfuko [wa fedha… ”
Imeuja katika upokezi mwingine:
”… wa dhahabu] ambao mkono wake ulikaribia kushindwa kuubeba, bali alishindwa [ambapo akamkabidhi nao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa juu ya mimbari yake]. [Akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, hii ni kwa ajili ya njia ya Allaah]. [Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaupokea]. [Abu Bakr akasimama na kujitolea, kisha ´Umar akasimama na kujitolea, kisha Muhaajiruun na Answaar wakasimama na kujitolea], kisha watu wakafuata mfululizo [katika kutoa swadaqah],
[Kuna ambao walijitolea dinari, wengine wakajitolea dirhamu, wengine wakajitolea hiki na kile], mpaka nikaona milundo miwili ya chakula na mavazi, mpaka nikauona uso wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukiangaza kana kwamba ni kipande cha dhahabu. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
”Yeyote atakayeanzisha Sunnah njema katika Uislamu, basi atakuwa na thawabu zake na [mfano wa] thawabu za watakaoitenda baada yake bila kupunguzwa kitu chochote katika thawabu zao. Na yeyote atakayeanzisha Sunnah mbaya katika Uislamu, basi atakuwa na dhambi yake na [mfano wa] dhambi za watakaoitenda baada yake bila ya kupunguziwa chochote katika dhambi zao. [kisha akasoma Aayah ifuatayo:
وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
”… na tunaandika yale waliyoyatanguliza na athari zao.”
[Akaendelea kusimulia: ”Akaigawa kati yao].”
Ameipokea Muslim (3/88, 89, 8/61, 62), an-Nasaa’iy (1/355, 356), ad-Daarimiy (1/126, 127), na at-Twahaawiy katika ”al-Mushkil” (1/93, 97), al-Bayhaqiy (4/175, 176), at-Twayaalisiy (670), Ahmad (4/357, 358, 359, 360, 361, 362) na Ibn Abiy Haatim pia katika ”Tafsiyr” yake, kama alivofanya pia Ibn Kathiyr (3/565). Ziada kabla ya mwisho ni yake. Mlolongo wake wa wapokezi ni Swahiyh. Vilevile ameipokea at-Tirmidhiy (3/377) ambaye pia ameisahihisha, Ibn Maajah (1/90) ambaye amejumuisha sentensi mbili kabla ya ziada iliyoashiriwa, pamoja na ziada mbili ndani yake. Kuhusu ziada ya kwanza ni ya al-Bayhaqiy, na kinachoifuata hadi ya nne ni yeye na Muslim. Ziada ya tano hadi ya nane ni ya al-Bayhaqiy, at-Twayaalisiy anayo ziada ya tano, ziada ya sita ni ya ad-Daarimiy na ya Ahmad. Muslim ana ziada mfano wa hiyo na vilevile at-Twayaalisiy na Ahmad. Ziada ya kumi, ya kumi na mbili, ya kumi na tano, na ya kumi na tisa ni ya al-Bayhaqiy. Ziada ya kumi na moja na ya kumi na saba ni ya at-Twahaawiy na Ahmad. Ziada ya kumi na nne ni ya at-Twayaalisiy, na ya kumi na sita na kumi na saba ni ya Muslim, at-Tirmidhiy, Ahmad na wengineo. Riwaya ya pili ni kutoka kwa an-Nasaa’iy na al-Bayhaqiy, na ya tatu ni kutoka kwa at-Twahaawiy na Ahmad[4].
[1] 36:12
[2] 04:01
[3] 59:18-20
[4] Angalizo!
Baadhi ya Ahl-ul-Bid´ah wanatumia hoja maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth hii:
”Yeyote atakayeanzisha Sunnah njema katika Uislamu… ”
juu ya mgawanyiko wao wa Bid´ah waliobuni na kwamba kuna Bid´ah nzuri na Bid´ah mbaya, hoja ambayo ni yenye dosari inayotokana na mgawanyiko batili, kama itakavyobainika kwa yeyote anayechunguza muktadha wa Hadiyth, kwani wao huficha na hawaitaji sababu yake. Hadiyth hiyo inahusu kuhimiza ufufuaji wa Sunnah, na sio kuhimiza kuanzishwa kwa Bid´ah.
Nukta nyingine ya kuraddi ni kwamba hata kama tutasema – kwa lengo la mahojiano – ya kwamba neno “Sunnah” lililotajwa katika Hadiyth kumekusudiwa Bid´ah, jumla ya kwanza imetaja Sunnah nzuri na jumla ya pili imetaja Sunnah mbaya. Ni jambo linalotambulika kwa Ahl-us-Sunnah ya kwamba mazuri na mabaya mategemezi yake ni kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kinyume na Mu´tazilah na wale wanaowafuata ambao wanaona mategemezi yake ni kwa mujibu wa wanaotumia akili. Ikiwa kuna kitendo kilichowekwa katika Shari´ah ambacho kimeelezwa kuwa ni Bid´ah nzuri na kukapokelewa dalili pambanuzi ndani ya Qur-aan na Sunnah juu ya hilo, basi hapo kutakuwa hakuna makinzao yoyote juu ya kwamba kitendo hicho kimewekwa katika Shari´ah. Kule kuitwa kwake kuwa ni ”Bid´ah” ni kwa mujibu wa lugha na si vyenginevyo. Mfano wa hilo ni maneno yake ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh):
”Ni Bid´ah nzuri iliyoje!”
Alisema hivo wakati wa kuhuisha usimamaji wa nyusiku za Ramadhaan kwa mkusanyiko baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alifanya hivo kwa kitendo na maneno yake. Vivyo hivyo inatumika kwa neno “Sunnah” na “mbaya” linapofasiriwa kuwa “Bid’ah”, inakuwa mbaya pale ambapo dalili za Kishari´ah zitapoonyesha hivo. Wewe unaona – na sifa zote njema anastahiki Allaah – namna zinavyodondoka dalili za wazushi wanaojengea hoja kwa Hadiyth hii kwa njia zote mbili zilizotajwa.
Unaweza kuona, himdi zote njema anastahiki Allaah, kwamba hoja ya wazushi inayoegemezwa juu ya Hadiyth hii ni batili katika njia zote mbili zilizotajwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kutoa tawfiyq.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 224-226
- Imechapishwa: 03/08/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 224-226
Imechapishwa: 03/08/2026
https://firqatunnajia.com/118-maiti-ananufaika-na-athari-njema-na-swadaqah-yenye-kuendelea/