Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا
”Na bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno kihakika.”[1]
Hata kama Mitume wote wako katika ngazi ya juu, lakini amefadhilisha zaidi baadhi juu ya wengine:
تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ
“Hao ni Mitume, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya wengine, miongoni mwao kuna aliyezugumzishwa na Allaah, na akawapandisha baadhi yao vyeo.”[2]
Allaah (´Azza wa Jall) amempa kila Mtume fadhilah yake maalum. Amemfadhilisha (Tabaarak wa Ta´ala) Ibraahiym na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam) kwa mapenzi ya hali ya juu na amemfadhilisha Muusa (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) kwa kumzungumzisha moja kwa moja bila mkatimkati. Muusa aliyasikia maneno yake. Allaah (Subhaanah) alimwita Muusa na akamnong´oneza. Yote haya yamemtokea Muusa (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam). Fadhilah hii amepwekeka nayo yeye. Zingatia namna Allaah alivyotilia mkazo hilo kwa kusema:
وتَكْلِيمًا
”… maneno kihakika.”
Amefanya hivo ili asiweko yeyote atakayesema kuwa ni mafumbo. Pindi alipotilia hilo mkazo kwa chanzo chake, ikafahamisha kuwa ni maneno ya kweli kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hapa kuna kumthibitishia maneno Allaah (´Azza wa Jall). Pia kuna kumthibitishia fadhilah Muusa (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam), kwa sababu yeye pekee ndiye mwenye sifa hiyo tofauti na Mitume wengine. Kwa sababu tu Mtume fulani anayo sifa maalum, haina maana kwamba anakuwa ni mbora kuliko Mitume wengine wote; hiyo ina maana ya kuwa yeye ni mbora kuliko Mitume wengine katika sifa hii pekee.
[1]4:164
[2]2:253
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 127
- Imechapishwa: 11/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)