ash-Shawkaaniy amesema katika ”Nayl-ul-Awtwaar” (4/79):
”Hadiyth za mlango huu zinajulisha kwamba swadaqah kutoka kwa mtoto humfikia mzazi wake baada ya kufariki bila ya kuwa na wasia kutoka kwao na thawabu zake huwafikia. Hivyo Hadiyth hizi zinapambanua maana ya jumla ya maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
“… na mtu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.”[1]
Lakini hakuna ndani ya Hadiyth za mlango huu isipokuwa ni swadaqah ya mtoto. Ni jambo limethibiti kwamba mtoto ni sehemu ya juhudi na kazi ya mzazi wake, hivyo hakuna haja ya kudai upambanuzi. Ama kutoka kwa wasiokuwa watoto dhahiri kutokana na ujumla wa Aayah za Qur-aan ni kuwa thawabu zake hazimfiki maiti. Hivyo yasimamishwe juu yake mpaka kupatikane dalili inayohitaji upambanuzi wake.”
Hii ndio haki ambayo inahukumiwa na kanuni za kielimu: kwamba Aayah inabaki katika ujumla wake na kwamba thawabu ya swadaqah na mengineyo humfikia mzazi kutoka kwa mtoto kwa sababu ni katika juhudi zake, kinyume na wasiokuwa watoto. Lakini an-Nawawiy na wengineo wamenukuu maafikiano kwamba swadaqah hutekelezwa kwa niaba ya maiti na thawabu zake humfikia. Hivi ndivyo walivyosema “maiti” kwa ujumla bila ya kufungamanisha na mzazi. Ikiwa maafikiano haya yamesihi basi ni upambanuzi wa jumla za Aayah alizozitaja ash-Shawkaaniy kuhusiana na swadaqah na kinachobaki katika jumla ni kama swawm, kusoma Qur-aan na ´ibaadah nyinginezo. Hata hivyo nina shaka kubwa juu ya usahihi wa maafikiano hayo kutokana na sababu mbili:
1 – Maafikiano kwa maana ya kimsingi haiwezi kuthibiti isipokuwa katika masuala yanayojulikana kwa lazima katika dini, kama walivyobainisha wanazuoni wakubwa, kama Ibn Hazm katika ”Usuwl-ul-Ahkaam”, ash-Shawkaaniy katika ”Irshaad-ul-Fuhuul”, Ustadh ´Abdul-Wahhaab katika kitabu chake ”Usuwl-ul-Fiqh” na wengineo. Imaam Ahmad ameashiria juu ya hilo katika maneno yake yanayojulikana ya kuraddi wale wanaodai maafikiano. Maoni hayo yamenakiliwa kutoka kwake na mwanawe ´Abdullaah bin Ahmad katika ”al-Masaa-il”.
2 – Nimepitia masuala mengi waliyonukuu maafikiano ndani yake ambapo nikakuta ndani yake kuna mitazamo tofauti inayotambulika. Hata nikakuta madhehebu ya jopo kubwa la wanazuoni yako kinyume na madai hayo ya maafikiano. Ningependa kutoa mifano mingi lakini itakuwa ndefu sana, basi sasa tutaje mfano mmoja tu: an-Nawawiy amenukuu maafikiano ya kwamba swalah ya jeneza haichukizwi katika nyakati zinazochukiza. Hali ya kuwa makinzano juu ya hili ni ya zamani na inayotambulika. Wanazuoni wengi wako kinyume na hayo maafikiano yanayodaiwa, kama ilivyotangulia kukaguliwa katika masuala ya 87. Kuna mfano mwingine utakuja punde kidogo – Allaah akitaka.
Baadhi yao wamefanya kipimo baina ya wasiokuwa mzazi kwa mzazi, nacho ni kipomo batili kwa njia nyingi:
1 – Kinapingana na ueneaji wa Qur-aan ikiwa ni pamoja na maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَمَن تَزَكَّىٰ فَإِنَّمَا يَتَزَكَّىٰ لِنَفْسِهِ
”Yeyote anayejitakasa, basi hakika anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake.”[2]
na nyinginezo katika Aayah ambazo zimeunganisha mafanikio na kuingia na Peponi kwa kufanya matendo mema. Hapana shaka yoyote kwamba mzazi hujitakasa kwa kumlea mtoto wake na kwa kumfunza na hivyo ana thawabu ya hilo, kinyume na wasiokuwa yeye.
2 – Ni kipimo chenye tofauti wazi, kwani Shari´ah imemfanya mtoto kuwa ni sehemu ya juhudi za mzazi, kama ilivyokuja katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Kwa hivyo si katika juhudi ya mtu mwingine. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ
“Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.” [3]
لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ
“Itapata [thawabu] iliyoyachuma na ni dhidi yake [kwa dhambi] iliyojichumia.”[4]
Haafidhw Ibn Kathiir amesema alipokuwa anafasiri maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

“… na mtu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.”
Kwa maana ya kwamba kama ambavyo haadhibiwi kwa dhambi za mwingine, basi vivyo hivyo hapati thawabu isipokuwa kwa alichokifanya yeye mwenyewe. Kutokana na Aayah hii Tukufu ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) na waliomfuata wamejengea hoja kwamba thawabu za kisomo cha Qur-aan haziwafikii wafu kwa sababu si katika matendo wala juhudi zao. Kwa sababu hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahimiza ummah wake juu ya hilo na wala hawakuelekeza kufanya hivo si kwa andiko la wazi wala ishara. Isitoshe hilo halikunukuliwa kutoka kwa yeyote katika Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Kama ingelikuwa ni kheri, basi wangelitutangulia kufanya hivo. Mlango wa ´ibaadah umewekewa mipaka ya Maandiko wala hairuhusiwi kuchanganya kipimo au maono.”
al-´Izz bin ´Abd-is-Salaam amesema katika ”al-Fataawa” (24/2 – mwaka wa 1692):
”Mwenye kufanya utiifu kwa Allaah (Ta´ala) kisha akamtumia thawabu zake aliye hai au maiti, basi thawabu hazimfiki, kwa sababu:

Basi akianza utiifu kwa nia ya kwamba ni kwa niaba ya maiti, basi hazipati thawabu hizo, isipokuwa katika yale ambayo yamebaguliwa na Shari´ah kama mfano wa swadaqah, swawm na Hajj.”
Kile alichosema Ibn Kathiyr kutoka kwa ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) ndio maoni ya wanazuoni wengi na kundi katika Hanafiyyah, kama alivyonukuu az-Zabiydiy katika ”Sharh al-Ihyaa’” (10/369).
3 – Kipimo hiki lau kingekuwa sahihi, basi kingepelekea kupendekezwa kuwapa wafu zawadi ya thawabu. Mambo yangelikuwa hivo basi Salaf wangelifanya, kwa sababu wao hapana shaka yoyote walikuwa na hima kubwa zaidi katika thawabu kuliko sisi. Hawakufanya hivyo, kama ilivyotangulia katika maneno ya Ibn Kathiyr. Hii inaonyesha kuwa kipimo kilichotajwa si sahihi, jambo ambalo ndio lengo.
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema katika ”al-Ikhtiyaaraat al-´Ilmiyyah”, uk. 54:
”Haikuwa miongoni mwa ada ya Salaf kwamba wanaposwali swalah ya kujitolea, wakafunga swawm ya kujitolea, wakahiji hijjah ya kujitolea au wakasoma Qur-aan, basi wanapeleka thawabu za mambo hayo kwa maiti wa waislamu. Basi haitakikani kuacha njia ya Salaf, kwani hiyo ndiyo bora na timilifu zaidi.”
Shaykh (Rahimahu Allaah) anayo maoni mengine katika suala hili ambayo ni kinyume na alichokitaja hapo juu kutoka kwa Salaf. Ameonelea ya kwamba maiti ananufaika na kila ´ibaadah kutoka kwa wengine. Maoni haya yamefanyiwa kazi na kutetewa na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake ”ar-Ruuh”, kwa hoja za kipimo ambacho tayari zimeonyeshwa ubatilifu wake. Hili ni kinyume na mwenendo wake uliozoeleka wa kutojitanua katika kipimo katika ´ibaadah ambazo halisi khaswa kama zinapingana na njia ya Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum).
Mukhtaswari wa maneno yake yametajwa na ´Allaamah Sayyid Muhammad Rashiyd Ridhwaa katika ”Tafsiyr-ul-Manaar” (8/254-270), kisha akamraddi Radd nzuri na yenye nguvu. Basi na amrejee yule aliyependa kujitanua katika suala hili.
[1] 53:39
[2] 35:18
[3] 74:38
[4] 02:286
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 219-221
- Imechapishwa: 03/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 219-221
Imechapishwa: 03/08/2026
https://firqatunnajia.com/116-kutetea-msimamo-wa-kwamba-thawabu-za-mtoto-pekee-ndio-humfikia-mzazi/