115. Ujuzi wa Allaah kwa watu na ujuzi wa watu kwa Allaah

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

95 –Amewafanya viumbe Wake wasiweze kuyazunguka.

MAELEZO

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anayajua yote yaliyo mbele ya viumbe na yote yaliyo nyuma yao, lakini hata hivyo viumbe hawawezi kumzunguka Yeye kwa ujuzi. Allaah (´Azza wa Jall):

وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ

“… wala hawakizunguki chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa akitakacho.”[1]

Allaah amekizunguka kila kitu kwa ujuzi:

لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا

”[Haya yote] ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu ni muweza na kwamba Allaah amekwishakizunguka kila kitu kwa ujuzi.”[2]

[1]2:255

[2]65:12

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 126
  • Imechapishwa: 11/11/2024