Swali 114: Hii leo wamekuwa wengi ambao wanajinasibisha na ulinganizi na hivyo jambo likapelekea kuwepo na ulazima wa kuwatambua wanazuoni wanaozingatiwa ambao wanasimamia jambo la kuuongoza ummah na vijana katika mfumo wa haki na wa sawa. Ni wanazuoni wepi ambao unawapendekeza vijana kurejea kwao?
Jibu: Kulingania kwa Allaah ni jambo la lazima. Elimu imesimama juu ya ulinganizi na jihaad baada ya elimu yenye manufaa. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ
” Naapa kwa al-‘Aswr. Hakika ya mwanaadamu bila ya shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana kwa kufuata ya haki na wakausiana kuwa na subira.”[1]
Imani kunakusudiwa kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), majina Yake, Sifa Zake na kumwabudu Yeye. Imani hiyo inazalisha matendo mema. Kwa sababu matendo ni lazima yajengwe juu ya elimu. Vivyo hivyo kulingania kwa Allaah, kuamrisha mema na waislamu kunasihiana. Mambo haya yanatakikana.
Lakini sio kila mtu anafaa kuyasmamia mambo haya. Mambo hayasimamiwi na yeyote isipokuwa tu wanazuoni na watu waliokomaa kimaono. Kwa sababu ni mambo mazito ambayo hayasimamii yeyote isipokuwa wale ambao wanastahiki. Ni jambo linalosikitisha ya kwamba mlango wa kulingania leo hii umekuwa ni mlango mpana ambao kila mmoja anaingia ndani yake. Wanaziita harakati zao kuwa ni kulingania na pengine wakawa ni wajinga wasiojua ni namna gani wanatakiwa kulingania. Matokeo yake wakaharibu zaidi kuliko wanavyotengeneza. Wamebeba hamasa na wanafanya mambo kwa papara na mkorogeko. Matokeo yake wakachangia madhara makubwa kuliko yale wanayotengeneza na wanayotaka kurekebisha. Pengine wakawa miongoni mwa wale wanaojinasibisha na ulinganizi na wakati huohuo wakawa na mipango na matamanio wanayolingania kwayo na wanataka kuyafikia kwa kutumia jina la ulinganizi. Wanazishawishi fikira za vijana kwa kutumia jina la ulinganizi na ghera ya dini na wakati huohuo anakusudia kuwapotosha vijana na kuwafanya waikimbia jamii, watawala na wanazuoni wao. Wanawajia kwa njia ya nasaha na kulingania, kama ilivyo hali ya wanafiki wa ummah huu ambao wanawatakia watu shari kwa kudhihirisha sura ya kheri. Allaah (Subhaanah) amesema kuhusu wanafiki waliojenga msikiti, kwa uinje ni kitendo kizuri, kwa nia ya kuwadhuru na kuwatawanya waislamu:
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا
”Na wale waliojenga msikiti kwa ajili ya kuleta madhara na kufuru na kufarikisha baina ya waumini na kuwa ngome kwa waliompiga vita Allaah na Mtume Wake hapo kabla. Na bila shaka wanaapa: Hatukukusudia isipokuwa jambo zuri. Na Allaah anashuhudia kwamba hakika wao ni waongo. Usisimame humo abadani!”[2]
Tukio hili tukufu linatubainishia kuwa sio kila ambaye anajidhihirisha kwa kheri na matendo mema anakuwa ni mkweli katika anayoyafanya. Pengine nyuma ya hayo akakusudia kinyume na yale anayodhihirisha. Wale wanaojinasibish na ulinganizi hii leo kuna wapotofu ambao wanataka kuwapotosha vijana na kuwapindisha kutokamana na haki na kuwagawanya waislamu na kuwaingiza ndani ya mitihani. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametutahadharisha kutokana na watu hawa pale aliposema:
لَوْ خَرَجُوا فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا خِلَالَكُمْ يَبْغُونَكُمُ الْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّاعُونَ لَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ
”Lau wangelitoka nanyi, wasingelikuzidishieni isipokuwa machafuko na wangeliharakia huku na huku baina yenu kukutakieni fitnah – na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza kwa makini [kwa ujasusi]. Na Allaah ni Mjuzi kwa madhalimu.”[3]
Kinachozingatiwa sio kule kujinasibisha au kile kinachodhihiri, bali kinachozingatiwa ni uhakika na matokeo. Kinachozingatiwa ni matukio. Watu wanaojinasibishwa wanapaswa kukaguliwa. Wamesoma wapi? Wamechukua elimu yao kutoka wapi? Wamekulia wapi? Ni ipi ´Aqiydah yao? Allaah (Ta´ala) amesema:
أَمْ لَمْ يَعْرِفُوا رَسُولَهُمْ فَهُمْ لَهُ مُنكِرُونَ
”Au hawajamtambua Mtume wao, basi wao ndio wanamkanusha?”[4]
Ni wajibu kuyakagua matendo yao na athari zao kwa watu. Wamezalisha kheri ipi? Matendo yao yamezalisha nini? Kwa hivyo ni lazima kuzikagua hali zao kabla ya kudanganyika na maneno yao na uinje wao. Hili ni jambo la lazima na khaswa katika wakati wa leo ambao walinganizi wa fitina wamekuwa wengi. Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaeleza walinganizi wa fitina na akasema:
”Walinganizi katika milango ya Motoni. Yule mwenye kuwaitikia wanamtupa humo.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Tueleze nao.” Akasema: “Ni watu wanaotokamana na sisi na wanazungumza lugha yetu.”[5]
Amewaita (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ni ”walinganizi”. Kwa ajili hiyo tunalazimika kuwa waangalifu juu ya hili na tusimwingiza kila mtu na kila ulinganizi. Haitoshi mtu kusema kuwa analingania kwa Allaah. Ni lazima ikaguliwe hali yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amefungamanisha ulinganizi iwe Kwake pale aliposema:
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي
“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata.”[6]
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu Aayah hiyo:
”Hapa amekokoteza kumtakasia nia. Kwa sababu kuna watu wengi wanaoita katika nafsi zao na si kwa Allaah (´Azza wa Jall).”
Hiyo imefahamisha kuwa kuna ambao wanalingania kwa asiyekuwa Allaah na Allaah (´Azza wa Jall) amesema kuhusu makafiri:
أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ
”Hao wanaitia katika Moto na Allaah anaitia katika Pepo na msamaha kwa idhini Yake.”[7]
Kwa hivyo ni lazima kuzikagua hali za walinganizi.
[1] 103:1-3
[2] 9:107-108
[3] 9:47
[4] 23:69
[5] al-Bukhaariy (3606) na Muslim (1847).
[6] 12:108
[7] 2:221
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 261-266
- Imechapishwa: 25/08/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 261-266
Imechapishwa: 25/08/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/114-namna-hii-ndivo-utapambanua-kati-ya-mlinganizi-mzuri-na-mlinganizi-mbaya/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)