Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Amesema wakati alipokuwa akieleza Kundi lililookoka:

“Ni lile litakalofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu.”[1]

MAELEZO

Bi maana lililookoka kutokana na Moto, kwa sababu kabla yake amesema:

”Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”

Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa juu ya kundi lililookoka na Moto, akasema:

“Ni lile litakalofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Hii leo, bi maana wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hicho ndio kigezo cha njia ya uokozi. Kwa sababu watu wengi wanadanganyika na wingi. Wanaona namna ambavyo watu wengi wanafuata jambo fulani na hatimaye wanaamua kupinda nao.

[1] Abu Daawuud (4596), at-Tirmidhiy (2641) na Ibn Maajah (3992). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (171).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 168
  • Imechapishwa: 10/09/2024