Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
Ole wake ambaye anamfanya Allaah (Ta´ala) kuwa mgomvi wake juu ya makadirio na kila mgonjwa wa moyo mwenye kujishughulisha na jambo hilo. Amejaribu kwa fikira yake kutafuta mambo ya siri yaliyofichikana na kuishilia kwa atakayoyasema kuwa mwongo na mtenda dhambi.
MAELEZO
Yule mwenye kupekua na kueneza mashaka kuhusu mambo yanayohusiana na makadirio ni mpinzani wa Allaah. Imani haisihi isipokuwa mpaka mtu aamini mipango na makadirio ya Allaah kwa mujibu wa ngazi zake nne na ilivyokuja ndani ya Qur-aan na Sunnah. Maswali, matatizo, mashaka na dhana hayatakiwi kuingia katika jambo hili. Mwenye kufanya hivo anavutana na Allaah (´Azza wa Jall). Wale waliopekua makadirio hawakufikia chochote. Badala yake wamekuwa wenye kudangana na mkanganyiko na kuiharibu ´Aqiydah yao. Mambo ya makadirio ni jambo ambalo analijua Allaah (´Azza wa Jall) pekee. Ni kitu hakitambuliki kwa kufikiria wala kwa akili. Usiikalifishe akili yako kitu isichokiweza. Akili imewekewa mpaka, haiwezi kukifahamu kila kitu. Kwa hivyo usiingize katika mambo isiyoyaweza. Mipango na makadirio ya Allaah ni siri ya Allaah katika viumbe Wake. Usipekui. Hujawajibishiwa jambo hilo, ulichowajibishiwa ni kufanya matendo, kutii na kujisalimisha. Yule mwenye kupekua na kupeleleza makadirio huishilia kwa atakayoyasema kuwa mwongo, bi maana mwongo na mtenda dhambi. Kwa sababu amefanya kitu ambacho hakuamrishwa nacho, na amepeleleza kitu ambacho hakimuhusu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 122-123
- Imechapishwa: 06/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)