Kwa hivyo jitahidini katika kufanya mambo ya utiifu na jiepusheni na madhambi na maasi ili mfuze kwa maisha mazuri ulimwenguni na malipo makubwa baada ya kufa. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Yule mwenye kutenda mema katika wanamme au wanawake – ilihali ni muumini – basi Tutamhuisha maisha mazuri na tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.”[1]

Ee Allaah! Tuthibitishe juu ya imani na matendo mema, Tuhuishe uhai mzuri, tukutanishe na wema. Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Mwisho!

[1] 16:97

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 229
  • Imechapishwa: 05/04/2024