110. Anakufuru hata kama hakujua kuwa kitendo ni kufuru

La kumi: Aayah inafahamisha kwamba mtu anakufuru hata kama hakujua kuwa kitendo hichi ni kufuru. Watu hawa hawakujua kuwa ni kufuru. Watu hawa walikuwa ni waumini. Amesema (Ta´ala):

قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

”Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (at-Tawbah 09:66)

Hawakujua kuwa ni kufuru. Pamoja na hivyo Allaah hakuwapa udhuru kwa hilo. Hivyo mtu anakufuru hata kama hakujua kuwa kitendo hichi ni kufuru. Vipi ikiwa mtu atakuwa mjuzi wa hilo? Khatari inakuwa kubwa zaidi. Jambo hili ni muhimu sana ya kwamba hakuna tofauti kati ya ambaye anayefanya kusudi na mfanya mchezo, kati ya mjuzi na mjinga katika jambo hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 139-140
  • Imechapishwa: 27/12/2018