74 – Yahyaa bin Ayyuub ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ja´far ametuhadithia: al-´Alaa’ bin ´Abdir-Rahmaan amenikhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Swadaqah haifanyi mali kupungua. Allaah (´Azza wa Jall) hamzidishii mja kwa kusamehe isipokuwa utukufu, na mja hatomnyenyekea Allaah (´Azza wa Jall) isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall) atamnyanyua.”[1]
75 – Abu Bakr bin Sahl at-Tamiymiy ametuhadithia: Ibn Abiy Maryam ametuhadithia: Yahyaa bin Ayyuub ametuhadithia: ´Abdullaah bin Zahr ametuhadithia, kutoka kwa ´Aliy bin Yaziyd, kutoka kwa al-Qaasim bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abu Umaamah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna yeyote isipokuwa yuko pamoja naye Malaika wawili na juu yake kuna lishiko ambalo wanalishika. Akitaka kujiinua, wao hulivuta na husema: ”Ee Allaah, mteremshe! Na akijinyenyekeza, husema: ”Ee Allaah, muinue kwa ajili ya hilo!”[2]
76 – Mahdiy bin Hafsw ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa Mutw´im bin al-Miqdaam as-Swan´aaniy, kutoka kwa ´Anbasah bin Sa´iyd al-Kalaa´iy, kutoka kwa Naswiyh al-´Ansiy, kutoka kwa Rakb al-Miswriy, ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Twubaa kwa yule aliyejinyenyekeza pasi na kuwa na upungufu wowote, akajidhalilisha pasi na kuwa masikini, akatoa mali aliyokusanya katika njia isiyo ya maasi, akawahurumia watu wa dhiki na umasikini na akachanganyika na wanazuoni na wenye hekima.”[3]
77 – al-Hasan bin Mansuur bin Sulaymaan al-Qurashiy ametuhadithia: Yahyaa bin Maymuun ametuhadithia: Abu Salamah al-Madaniy amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali kwetu Qubaa´ hali ya kuwa amefunga. Tukamletea kikombe cha maziwa na tukatia humo asali kidogo. Alipokipandisha na kuonja akahisi ladha ya asali. Akasema: “Hii ni nini?” Tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah, tumeweka kiwango kidogo cha asali.” Akakiweka chini na akasema: “Ama kwa hakika siiharamishi. Na mwenye kujinyenyekeza, basi Allaah humnyanyua. Na mwenye kujivuna, basi Allaah humteremsha chini. Na mwenye kuwa na wastani, basi Allaah humtajirisha. Na mwenye kubadhirisha, basi Allaah humfukarisha. Na mwenye kumtaja Allaah sana, basi Allaah humpenda.”
78 – Ahmad bin Ibraahiym bin Kathiyr al-´Adawiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Idriys ametuhadithia: Ibn ´Ajlaan amenihadithia, kutoka kwa Bukayr bin ´Abdillaah bin al-Ashajj, kutoka kwa Ma´mar bin Abiy Habiybah, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Adiy bin al-Khayyaar: Nimemsikia ´Umar bin al-Khattwaab akisema:
”Hakika mja anapojinyenyekeza kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall), basi Allaah humuinua lishiko lake na husema: “Ishi vizuri, Allaah amekuinua!” Na akijivuna na kupita mipaka yake, Allaah humponda ardhini na husema: “Ondoka, Allaah akudhalilishe!” Basi huwa mkubwa machoni mwake mwenyewe lakini mdogo machoni mwa watu mpaka awe kwao kama nguruwe. Enyi watu, msimchukize Allaah kwa waja Wake.” Wakauliza: ”Hilo linakuwa vipi?” Akasema: ”Mmoja wenu husimama kuwa imamu kisha akawarefushia na hivyo huwafanya wachukie kile wanachofanya.”
[1] Muslim (2588), at-Tirmidhiy (2029) na Ahmad (2/235).
[2] Tazama ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2895) na “as-Swahiyhah” (538) vya al-Albaaniy.
[3] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1368).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 96-104
- Imechapishwa: 29/01/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 96-104
Imechapishwa: 29/01/2026
https://firqatunnajia.com/11-swadaqah-na-kujinyenyekeza/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket