al-Khaliyl bin Ahmad amesema:

“Nilimwendea Abu Rabi’ah al-Araabiy, ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu wajuzi zaidi ninayemjua, alipokuwa juu ya paa lake. Alipotuona alitusalimia kwa ishara na akasema: “Inukeni (استووا).” Hatukujua alimaanisha nini, ambapo mzee aliyekuwa naye akasema: “Anakuambia muinuke.” al-Khaliyl amesema: ”Hiyo ndio asili ya maneno Yake (Ta´ala):

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ

”Kisha akalingana juu ya mbingu iliali ni moshi… ”[1]

Kwa maana ya kwamba akawa juu na kuinuka.”[2]

Bila kujali kama kulingana kunaambatana na viambishi (إلى) au (على), maana yake ni kuwa juu na kuinuka. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wale wanaosema kuwa maana yake ni kwamba amekusudia wanajengea hoja kwa maneno Yake (Ta’ala):

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ

”Kisha akalingana juu ya mbingu iliali ni moshi… ”

Kwa sababu kihusishi (إلى) kinakusudia lengo. Licha ya hayo matumizi hayo hayajulikani katika lugha pia. Wala hakuna yeyote katika wafasiri wa Qur-aan wa Salaf aliyesema hivo. Bali wafasiri wa Salaf wamezungumza kwa kuafikiana kinyume na hivo, kama nilvyotangulia kutaja mifano ya hilo.”[3]

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja maafikiano ya Salaf juu ya jambo hilo[4].

Haya yalikuwa ni maelezo mafupi ya ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa’ah kuhusu sifa hiyo. Yeyote anayetaka kujua zaidi kuhusu sifa hiyo basi anaweza kurejelea vitabu vinavyohusika, ambavyo ni vingi sana. as-Safaariyniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wanazuoni wameandika vitabu vingi juu ya mada hiyo. Wamefanya kila wawezalo kuthibitisha  Ujuu na Kulingana na wakazindua juu ya hilo kwa Aayah na Hadiyth za Qur-aan. Baadhi wameyanukuu mapokezi kwa cheni za wapokezi wake, wengine wameziruka na kutosheka na matamshi yenye manufaa. Wengine wameingia ndani zaidi na kuandika kwa kina, wengine kwa ufupi, wengine wamekuwa wastani na wengine wamechuja tu. Miongoni mwa vitabu hivyo ni “Mas-alat-ul-´Uluww” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, “Ithbaat-ul-‘Uluww” cha Imaam Muwaffaq-ud-Diyn, ambaye pia ameandika tungo nyingine kwa mujibu wa Ahl-us –Sunnah, “al-Juyuush al-Islaamiyyah” cha mhakiki Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah” na “Kitaab-ul-´Arsh” cha Haafidhw Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy. Itakuwa vigumu sana kuvitaja vitabu hivyo vyote – na Allaah (Ta´ala) ndiye Mwenye kuwafikisha.”[5]

[1] 41:11

[2] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 171.

[3] Majmuu´-ul-Fataawaa (5/521).

[4] Mukhtaswar-us-Swawaa´iq al-Mursalah, uk. 320.

[5] Lawaamiy´-ul-Anwaar al-Bahiyyah (1/195-196).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 24-26
  • Imechapishwa: 28/11/2025