Miongoni mwa alama za Qaadiyaaniyyah kubwa ni kwamba, wanapoanza ulingano wao basi huanza kwa kuthibitisha kuwa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshakufa. Wakiweza kuyakita hayo kwa wasikilizaji, ndio wanaenda kwenye hatua ya pili; wanaanza kutaja  Hadiyth zinazozungumzia kushuka kwa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hujidhihirisha kama wenye kuziamini, lakini ni haraka sana huanza kuzipindisha maana. Muda wa kuwa wameshathibitisha kufa ´Iysaa, basi wanazipindisha maana Hadiyth hizo kwamba kilichokusudiwa ni kushuka kwa mtu mfano wa ´Iysaa. Naye si mwingine ni Mirza Ghulaam Ahmad al-Qaadiyaaniy.

Wanazo tafsiri za kimakosa kama hizo nyingi mno jambo ambalo linatufanya kuthibitisha kwa kukata kabisa kwamba watu hawa ni katika kundi la Baatwiniyyah la kikafiri. Tutaashiria baadhi ya ´Aqiydah zao huko mbele – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 23
  • Imechapishwa: 16/09/2024