11. Mke mwema anatakiwa kuwa muadilifu kwa watoto wake

Katika sifa za mke mwema ni kwamba Allaah Akimneemesha kwa kumpa watoto anatakiwa kufanya uadilifu kati yao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu. Fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu.”

Hadiyth hii imepokelewa na Abu Daawuud[1] na kumekuja Hadiyth nyingi kwa maana kama hii.

[1] 3544. Imepokelewa na an-Nu´maan bin Bashiyr (Radhiya Allâhu ´anh). al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (1240).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 41
  • Imechapishwa: 12/08/2018