Swali: Ni ipi hukumu ya mfungaji kutumia sprei mchana wa Ramadhaan kwa sababu ya maradhi ya pumu na mfano wake?

Jibu: Hukumu yake ni kufaa iwapo atalazimika kufanya hivo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“… na ilhali ameshakubainishieni yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.”[1]

Jengine ni kwa sababu hilo halifanani na kula na kunywa. Hilo limefanana na kuchota damu kwa sababu ya kipimo au sindano isiyokuwa ya lishe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 11
  • Imechapishwa: 31/03/2021