11. Maneno yanayojaza yalio baina ya mbingu na ardhi

18 – Abu Maalik al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

الْحَمْدُ لِلَّهِ

“Himdi zote njema ni za Allaah.”

inajaza mizani.

وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ

“Allaah ametakasika kutokana na mapungufu na himdi zote njema ni za Allaah.”

yanajaza kilicho baina ya mbingu na ardhi.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hadiyth inafahamisha fadhilah za Tasbiyh na Tahmiyd. Kwa maana nyingine ubora wa kusema “Subhaan Allaah” na “Alhamdulillaah”. Kwa sababu yanajaza mizani na yanajaza yalio baina ya mbingu na ardhi. Kwa msemo mwingine yangelikuwa ni gramu basi yangelijaza yalio baina ya mbingu na ardhi, kama ilivyopokelewa katika kupimwa uzito matendo.

[1] Muslim (223).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 24
  • Imechapishwa: 01/10/2025