11 – Kuwatendea wema wazazi na kuzitekeleza haki zao
Inakupasa, ee dada yangu wa Kiislamu, kuwatendea wema wazazi wako. Kwani haki ya wazazi ni kubwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameambatanisha kuwatendea wema pamoja na kumwabudu. Amesema (Ta´ala):
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا
“Mola wako ameamrisha ya kwamba, msiabudu yeyote isipokuwa Yeye pekee; na kuwatendea wema wazazi wawili.”[1]
Hakika ni miongoni mwa wema kuwatendea ihsani wa kina aina, kuwatekelezea haja zao, kuzungumza nao kwa upole na adabu, kuwaombea du´aa wakati wa uhai wao na baada ya kufa kwao.
Miongoni mwa makosa yanayosikitisha ni kwamba utamkuta binti amekaa kitako na mama yake ndiye anamhudumia. Miongoni mwa makosa mengine yanayosikitisha ni kwamba utamkuta msichana mwingine anayewanyanyulia sauti wazazi wake. Allaah amekataza dogo zaidi kuliko hilo. Amesema (Ta´ala):
فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا
“… basi usiwaambie ´Ah` na wala usiwakemee na waambie maneno ya heshima.”[2]
[1] 17:23-24
[2] 17:23
- Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 18-19
- Imechapishwa: 10/02/2026
11 – Kuwatendea wema wazazi na kuzitekeleza haki zao
Inakupasa, ee dada yangu wa Kiislamu, kuwatendea wema wazazi wako. Kwani haki ya wazazi ni kubwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameambatanisha kuwatendea wema pamoja na kumwabudu. Amesema (Ta´ala):
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا
“Mola wako ameamrisha ya kwamba, msiabudu yeyote isipokuwa Yeye pekee; na kuwatendea wema wazazi wawili.”[1]
Hakika ni miongoni mwa wema kuwatendea ihsani wa kina aina, kuwatekelezea haja zao, kuzungumza nao kwa upole na adabu, kuwaombea du´aa wakati wa uhai wao na baada ya kufa kwao.
Miongoni mwa makosa yanayosikitisha ni kwamba utamkuta binti amekaa kitako na mama yake ndiye anamhudumia. Miongoni mwa makosa mengine yanayosikitisha ni kwamba utamkuta msichana mwingine anayewanyanyulia sauti wazazi wake. Allaah amekataza dogo zaidi kuliko hilo. Amesema (Ta´ala):
فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا
“… basi usiwaambie ´Ah` na wala usiwakemee na waambie maneno ya heshima.”[2]
[1] 17:23-24
[2] 17:23
Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 18-19
Imechapishwa: 10/02/2026
https://firqatunnajia.com/11-kuwatendea-wema-wazazi/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket