Vilevile inahusiana na yale yaliyonakiliwa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa Maswahabah hata haikutajwa kwamba wamechukua kutoka kwa watu wa Kitabu. Pindi wanafunzi wa Maswahabah watatofautiana basi hakuna maoni ya yeyote yatayokuwa ni hoja dhidi mtu mwengine. Kwa upande mwingine jambo lililonakiliwa kwa usahihi kutoka kwa baadhi ya Maswahabah linautuliza moyo zaidi kuliko yaliyonakiliwa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa Maswahabah. Kwani kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba Swahabah huyo amelisikia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au kutoka kwa mtu ambaye amesikia kutoka kwake. Jengine ni kwamba Maswahabah walisimulia machache kutoka kwa watu wa Kitabu kuliko walivyofanya wanafunzi wao. Kwa kuongezea ni kwamna Maswahabah wanathibitisha yale wanayoyasema. Basi itawezekanaje kusema kwamba wamechukua elimu yao kwa watu wa Kitabu na hali wamekatazwa kuwasadikisha?

Suala hapa kukhitimisha ni kwamba makinzano kama haya ambayo haiwezekani kuthibitisha usahihi wake na ambayo maono yake si lazima kuyanukuu ni kama elimu ya Hadiyth iliyosimuliwa ambayo hakuna dalili juu ya usahihi wake na mfano wa hayo. Aina ya kwanza, ambayo usahihi wake unaweza kuthibitishwa, ipo katika yale ambayo mtu anayahitajia – na himdi zote njema zinarejea kwa Allaah. Mara nyingi hunukuliwa elimu katika tafsiri ya Qur-aan, Hadiyth na vita kutoka kwa Mtume wetu na Mitume wengine (Swalla Allaahu ‘alayhim wa aalihi wa sallam). Nukuu sahihi inazuia hayo. Lengo ni kwamba nukuu zinazohitajika katika dini zimewekewa dalili na Allaah ili kubainisha kilicho sahihi na kisicho sahihi.

  • Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 31/03/2025